Katika
mfululizo wa matamasha ya Airtel Yatosha yanayoendelea mikoa mbalimbali nchini
, Kampuni ya Airtel mwishoni mwa wiki hii itatoa burudani pamoja na
utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wakazi wa temeke , jijini Dar es
salaam katika viwanja vya Mbagala Zakhem siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe
4 na 5 mwenzi May 2013.
Tamasha
la Airtel yatosha litapambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya
wakiwemo , Sir Juma Nature akiwa na kundi la wanaume halisi, Madii akiwa na
kundi zima la tiptop connection, pamoja na wakali wa hipop Fid Q ,
Roma Mkatoliki na Ney wa mitego .
Akiongea
kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando amesema,
tumefanya matamsha ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini lengo hasa
likiwa ni kutoa elimu kuhusu huduma zetu ikiwemo Airtel yatosha na
kuwaunganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano bora na bei nafuu wa
Airtel.
Na
mwishoni mwa wiki hii tunawafikia wateja na wakazi mkoa wa Dar es salaamawa na
kuwapa nafasi ya kusajili namba zao, kujiunga na huduma ya Airtel
yatosha, Airtel Money na internet ya kasi ya 3.75G, kupata elimu
kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Airtel na kuunganishwa na mtandao wa Airtel
kwa wale wateja wapya.
Kiingilio
ni BURE, Njoo na kitambulisho chako upate kuunganishwa na huduma zetu na
kupata burudani kutoka kwa wasanii mahiri wa kizazi kipya Aliongeza Mmbando.
Kujiunga
na huduma ya Airtel Yatosha mteja anatakia kupiga *149*99# na kuunganisha
moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda
na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.
No comments:
Post a Comment