Baadhi
ya wafanyakazi kutoka Wizara mbalimbali za Serikali na Taasisi Binafsi
wakiwa katika foleni wakijiandaa kuanza maandamano kuelekea kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Sherehe za
Mei Mosi, ambapo katika Sherehe hizo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidick, huku sherehe hizo kitaifa
zikifanyika Kitaifa Mkoani Mbeya, na Mgeni Rasmi huko ni Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mgeni
rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akiwa meza kuu
na baadhi ya viongozi wengine wakati wakisimama kupokea maandamano
hayo.
Wafanyakazi
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF, wakipita mbele ya jukwaa kuu na
maandamano na mbwembwe za kucheza Kiduku, wakati wa sherehe hizo.
Wafanyakazi wa TALGWU, wakipita mbele ya jukwaa kuu na Bango lenye ujumbe.
Twiga Cement wao walikuwa wakipromoti bidhaa yao tu bila hata bango lenye ujumbe kuhusiana na sherehe hizo.
Maandamano yakiendelea kupita mbele ya jukwaa kuu.
Maandamano yakipita mbele ya jukwaa kuu........
'Watenda Haki' wakipita na bango lao mbele ya jukwaa kuu......SOURCE:SUFIANMAFOTO BLOG
No comments:
Post a Comment