Habari na Picha na Francis Godwin
WAZIRI mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema kuwa mbali ya kuwa yeye si tajiri ila bado ataendelea kufanya kazi yake kwa ukaribu zaidi na jamii ikiwa ni pamoja na kushirikiana na marafiki zake kusaidia na kuwataka wale wote wenye kusema dhidi yake kuendelea kusema ila hatarudi nyuma katika kutoa misaada kama njia ya kutafuta baraka za Mungu.
Lowassa ambae pia alikabidhiwa tuzo ya heshima kwa ajili ya kuendeleza kulipigania Taifa la Tanzania ,huku mwenyewe akichangia kiasi cha Tsh milioni 15 na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akichangia milioni 9 kati ya fedha zote zaidi ya Tsh milioni 75 zilizochangwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kanisa la OPC mkoani Iringa kama njia ya kuhamasisha amani katika Taifa ametaka watanzania kuwapuuza wale wote wanaoeneza siasa za uchochezi .
“Nataka kuwaomba leo wachukieni wachochezi na pia niwaelezeni kuwa mimi si tajiri ila nina utajiri wa watu na ushawishi na ninafanya mambo haya ili kumbukumbu yangu iweze kuandikwa Mbinguni na nimekuwa nikialika watu wengi na nimekuwa nikifika wacha wenye kusema waseme watasema ila usiku watalala wenyewe ….sitaacha kusaidia kwa kuogopa kusemwa”
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na kituo cha maombezi na uponyaji mkoani Iringa Overcomers Power Center (OPC) na kufanyika katika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa leo Lowassa alisema kuwa yeye si tajiri kama ambavyo watu wanavyofikiri ila amekuwa akipewa nguvu na rafiki zake ambao wamekuwa wakimuunga mkono pindi anapoalikwa katika hafla mbali mbali.
“Nataka kwanza kuwashukuru ndugu zangu wa mkoa wa Iringa na napenda kumshukuru zaidi Askofu Dkt Boaz Sollo kwa kunialika mkoani Iringa …..ila napenda kuwaeleza kuwa si kwamba nachangia michango mbali mbali katika jamii kama mimi ni tajiri ila mimi ni mtumishi nisiye na faida na nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu Pia nawashukuru sana wabunge wenzangu ambao wamepata kushiriki name leo katika ziara hiyo akiwemo mbunge machachari bungeni Deo Filikunjombe , Kagi Lugola na dada yangu Ritta Kabati bila kumsahau mbunge Mendradi Kigola kwa kuungana nami leo naamini nao wamepanda mbegu bora”.
Lowassa alisema kuwa anatambua bado ana mialiko migi sana na lazima anaifanyia kazi mialiko yote kama ambavyo jamii imepata kumwalika na kuwa hata hatua ya mkoa wa Iringa kumpa tuzo hainamanishi kuwa ni mwisho wa yeye kualikwa.
Hata hivyo Lowassa alisema kuwa kwa upande wake anapongeza jitihada za askofu Dkt Sollo kwa kuwa na mipango na mitazamo ya kulisaidia Taifa kwa kuanzisha ujenzi wa kanisa kwa ajili ya kudumisha amani na kwenda mbali zaidi kwa kuanzisha kituo cha radio Overcomers Fm chambo ambacho kitatumika kudumisha amani ya mkoa wa Iringa na Taifa pia
Kuhusu amani ya Taifa la Tanzania LOwassa alisema kuwa alikuwa ni miongoni mwa watu walioalikwa Kenya katika sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta ila sehemu kubwa ya wote waliotoa salam zao walitumia muda mwingi kupongeza vyombo vya habari kwa kulinda amani na hivyo kuvitaka vyombo vya habari za Tanzania na wanahabari kuendelea kuandika habari bila kuhatarisha amani ya Taifa
“Tusiruhusi amani ya nchi yetu iyumbishwe na mtu awaye yeyote na kila mtanzania anapaswa kulinda amani hii kwa nguvu zote ….Nawaombeni wanahabari tunzeni amani yetu…wapuuzeni wale wote wanaoch0chea machafuko katika Taifa hili ….tuachane na udini wala ukabila katika taifa letu ila “
Katika hatua nyingine Lowassa aliwapongeza wabunge wa CCM ambao wameendelea kupigania wanyonge bungeni akiwemo Deo Filikunjombe mbunge wa Ludewa na mbunge wa jimbo la Mwibara Kagi Lugola kuwa ni miongoni mwa wabunge ambao amekuwa akiwapenda kutokana na kusema kweli bungeni.
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe alisema kuwa mbali ya kutoa ahadi ya kuchangia kiasi cha Tsh milioni 9 ila bado atamwalika Lowassa jimboni kwake Ludewa na kuwa kanisa hilo la OPC halijakosea kumpa tuzo ambayo ni ramani ya Tanzania kutokana na Lowassa kuwa ni mtu wa watu mpendwa na watu na kuwa tuzo hiyo ina maana kubwa na hawajakupa ramani ya jimboni kwako Monduli
Filikunjombe alimtaka Lowassa kuendelea kuchapa kazi na kuwa hajakosea kuwaalika wao kwani bungeni kuna wabunge zaidi ya 300 ina amewachagua wao pekee ni jambo la kumshukuru na kumfananisha L0wassa na mti unaopigwa mawe kuwa ni mti wenye matunda
“Nakuomba Lowassa simama Imara sisi wana Iringa tupo nyuma yako na niseme tuna kazi kubwa ya kuifanya katika Taifa hili kubwa ni kumwomba Mungu na makanisa na dini zote kuungana katika maombi zaidi kwani vita ni kubwa mbele “
Kwa upande askofu Dkt Sollo mbali ya kumpongeza Lowassa bado alisema kuwa wao kama kanisa wataendelea kumwombea afya njema na kuona kuwa mambo yake yanafanikiwa na ndio maana ya kumpa tuzo hiyo ya heshima.
Sollo alisema kuwa mchango wa TSh milioni 15 ulioahidiwa na Lowassa na ule wa milioni 9 ulioahidiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ni mchango ambao wao wanaupongeza na kuwapongeza wabunge wengine akiwemo Ritta Kabati aliyeahidi Tsh milioni 2 ,Benki ya wananchi Mufindi milioni 2 , mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu milioni 2 mfanyabiashara Salim Abri milioni 1 na wengine wengi ambao wamepelekea kupata zaidi ya Tsh milioni zaidi ya 75 pesa taslim na ahadi .
No comments:
Post a Comment