Timu ya soka na Netiboli za Waandishi wa Habari za
michezo nchini, Taswa FC na Taswa Queens zimemaliza maadhimisho ya sikukuu ya
Pasaka kwa vishindo baada ya kuwatambia wageni wao, timu ya Kiliflora ya
Arusha.
Katika mchezo wa soka, Taswa FC iliibuka kwa ushindi
wa mabao 4-1 wakati katika mchezo wa netiboli uliochezwa kwenye uwanja huo huo,
Taswa Queens iliyokuwa inacheza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 18 iliibuka
na ushindi wa mabao 28-8.
Taswa FC ilianza mechi hiyo kwa kasi na kufana
mashambulizi ya mengi hata hivyo, washambuliaji wake, Julius Kihampa na Shafii
Dauda walikosa mabao mengi ya wazi.
Katika mechi hiyo, kipa wa Taswa FC, Said Seif
alikuwa ‘likizo’ kufuatia safu ya ulinzi chini ya Muhidin Sufiani, Fred Mweta,
Sweetbert Lukonge, Fred “Chuji” Mbembela kuwa imara muda wote huku safu ya
kiungo ilichezwa na Ali Mkongwe, Wilbert Molandi, Majuto Omary na Evarist
Hagila kutotoa mwanya kwa Kiliflora kupenya na kupeleka mashambulizi.
Baada ya kosa kosa hizo, Taswa FC iliandika bao lake
la kwanza katika dakika ya 24 kufuatia gonga safi za Majuto “Ronaldo De Lima” Omary
na Ali Mkongwe kabla ya mpira kumfikia Hagila na kuuweka kimiani.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya Kiliflora na
kujikuta wakipachikwa bao la pili kupitia kwa Dauda baada ya pasi nzuri ya
Wilbert Molandi aliyecheza vyema na
Sweetbert Lukonge na kufanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0 mpaka mapumziko.
Taswa Fc ilifunga bao la tatu kupitia kwa Hagila
baada ya pasi kupata pasi safi ya Fred Mbembela ‘Chuji’ na baadaye Dauda
kufunga la bao la nne kufuatia ngazi nzuri ya Majuto.
Katika netiboli, ikiongozwa na Imani Makongoro
aliyecheza nafasi ya (GS), Taswa Queens iliifunika kabisa Kiliflora Queens
baada ya kuongoza kwa 16-3 hadi Mapumziko.
Wachezaji wengine wa Taswa Queens waliocheza mechi
hiyo mbali ya Imani ni Oliver (mwananchi), Sada Ayoub, Johari William, Elizabeth Mbassa, Shaarifa
Mustapha wote wakitokea Business Times. Timu hiyo ilikuwa chini ya makocha,
Amina Mussa (BTL) na Zainab Ramadhan (TBC).
No comments:
Post a Comment