Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa
ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa
itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mabadiliko
hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya
sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa
usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya
mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.
Ligi
hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal
Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati
Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.
No comments:
Post a Comment