“Lovers
& Friends”
- Kipindi cha Power Jam ya East Africa Radio kinakuletea 'Lovers & Friends'.
- Katika t-shirt zetu za TZ, unadhani ni chata ipi ya mtaa inayofanya poa?Kama unajibu tuletee Ijumaa ya tarehe 12, mwezi huu ndani ya Club Maisha.
- Siku ya 'Lovers & Friends', Power Jam itakuwa inatafuta chata kali ya t-shirt hapa town...kwa hiyo tinga katika t-shirt yako na tukutane pale kwanzia saa 3 usiku!
- Kwa wale ambao mtataka kushindanisha t-shirt zenu basi dondosha t-shirt yako yenye chata yako hapa ofisi za East Africa Radio ili upate kuingia kwenye mchakato huu mkubwa hapa town.
- Ukileta t-shirt yako hakikisha unaandika na kuacha jina lako kamili, namba zako za simu na e-mail kama unayo.
- T-Shirt 50 safi na fresh za kwanza kuletwa ofisini kwetu ndio zitashindanishwa tu!
- Usikose 'Lovers & Friends' , ni Ijumaa ya mwezi huu, tarehe 12 na getini ni elfu 10 tu!
- Huu sio usiku wa kukosa njoo umependeza na umetinga t-shirt yako kali maana burudani itakuwa balaa...Dj Summer na Dj AD aka 'Mafuvu' nao watafanya yao!
- Chata yako ni kali kushinda yangu.......njo tuone!
No comments:
Post a Comment