Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti kutoka
NIMR, Dk. Julius Massaga akitoa taarifa juu ya mradi unaoendeshwa chini ya NIMR
ambao umelenga kupambana na kupunguza vifo vinavyotokana na Malaria ndani ya
Wilaya ya Pangani kwa kutumia wahudumu wa afya ya Msingi kwa kutumia dawa ya
mseto ya ALU. Zaidi ya watoto elfu kumi walio na umri kati ya miezi 3 hadi miaka
5 walifaidika kwa kupata matibabu ya ugonjwa wa Malaria bure wilayani Pangani
katika awamu ya kwanza ya mradi.
KATIKA jitihada za kuhakikisha vifo vya watoto
wadogo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Malaria nchini, zaidi ya watoto elfu
kumi walio na umri kati ya miezi 3 hadi miaka 5 wamepatiwa matibabu bure kutoka vijiji 16
vya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Hayo yamebainika wakati wa Mkutano wa 27 wa
Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) unaofanyika
sambamba na na Kongamano la pili la Wanasayansi watafiti barani Afrika, kwa
siku nne jijini Arusha Tanzania.
Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti kutoka
NIMR, Dk. Julius Massaga alisema zoezi hilo lilifanikiwa kupitia wahudum,u wa
afya za Msingi na liliwahusu zaidi watoto waishio katika maeneo ambayo
upatikanaji wa huduma za afya ni duni.
Dkt.Massaga amesema watoto hao wamefaidika kwa
kupatiwa matibabu bure kupitia mradi unaoendeshwa chini ya NIMR ambao umelenga
kupambana na kuepusha vifo vinavyotokana na Malaria ndani ya Wilaya ya Pangani.
Mradi huo ambao ni endelevu ulianza rasmi mwaka 2008 na sasa unaingia kwenye kipindi cha pili cha mapambano dhidi ya Malaria na NIMR inahakikisha kuwa wahudumu wanapatiwa mafunzo ya kuhakikisha kuwa dawa hazitolewi bila mgonjwa kupafanyiwa vipo vya Malaria kama ilivyokuwa awali ambapo dawa zilikuwa zikitolewa bila vipimo.
NIMR ilitoa mafunzo na vifaa kwa wahudumu wa
Afya 59 lakini kwa uchache wao wameweza kuleta mafanikio kwa mradi huo na jamii
kwa ujumla.
Awamu ya pili ya mradi huo inataraji kuanza
mwezi Mei 2013 hadi Mei 2014 na utasaidia pia kutoa elimu dhidi ya Malaria kwa
kaya mbalimbali.
Watafiti wanasayansi zaidi ya 300 wa magonjwa ya binadamu na wanyama kutoka Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanashiriki kongamano hilo na mada 174 zinawasilishwa na kati ya mada hizo 42 zinajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta za Afya,Mifugo,Wanyapori na Mazingira katika kuthibiti magonjwa ya mlipuko.
Watafiti wanasayansi zaidi ya 300 wa magonjwa ya binadamu na wanyama kutoka Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanashiriki kongamano hilo na mada 174 zinawasilishwa na kati ya mada hizo 42 zinajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta za Afya,Mifugo,Wanyapori na Mazingira katika kuthibiti magonjwa ya mlipuko.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo la pili barani
Afrika la Afya moja ni Mabadiliko ya mandhari ya tafiti za afya barani afrika.
Dk Martha Lemnge ambaye ni Mkurugenzi NIMR Tanga na Mshindi wa Tuzo ya Mtafiti bora wa Afya wa Mwaka 2013 akitoa mada juu ya ugonjwa wa Malaria.
Watafiti
Mbalimbali wa magonjwa ya Binadamu wakiwa katika mijadala juu ya
udhibiti wa ugonjwa wa Malaria nchini Tanzania na Afrika. Mada
mbalimbali zilitolewa na watafiti hao.
Mtoa mada katika mpango wa Afya Moja barani Afrika akitoa mada yake juu ya Magonjwa yasiyopewa kipaumbele wakati wa mdahalo huo ambao ni moja ya midahalo inayoendelea katika Mkutano Mkuu wa 27 wa NIMR na kongamano la Pili la Watafiti barani Afrika linaloendelea jijini Arusha.
Sehemu ya watafiti wanasayansi mbalimbali wa magonjwa ya binadamu na wanyama wakifuatilia mada katika mdahalo wa Afya Moja.
Mmoja wa watafiti akitoa mada juu ya upatikani wa maji safi na salama.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania
(NIMR) Dk. Mwele Malecela (kushoto) akiwa pamoja na Dk. Mercy Chiduo
katika moja ya midahalo ya wanasayansi juu ya maji safi na salama .
Badhi ya wanasayansi kutoka taasisi na nchi mbalimbali wakifuatilia mada juu ya maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment