Mshindano makubwa na mazuri ya GUINNESS® FOOTBALL™
CHALLENGE yamekuwa yakiwasisimua na kuwafurahisha watazamaji wake kwa wiki tano
zilizopita.Sasa mashindano ya Pan-African yataanza kuoneshwa katika televisheni
za ITV na Clouds TV kuanzia kesho tarehe
24 April, 2013 saa 3:15 ITV na 2:15 Clouds TV. Sasa timu kutoka Cameroon, Ghana,
Uganda, Kenya na Tanzania zitakutana uso kwa uso kushindana ili kujua ni
nani ana maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu, hata kuvishwa ubingwa wa Pan-African.
Washiriki kutoka Afrika yote waliowashinda
wapinzani zao ili kuwakilisha nchi zao sasa watakutana na timu bora za
Pan-African ambazo zina maarifa na ujuzi zaidi. Katika hatua hii ya robo
fainali washiriki wanawania kushinda hadi dola za Kimarekeni 250,000.
Kila timu sasa itacheza kuwakilisha
nchi yake na kuonesha uwezo wao katika kusakata kabumbu. Washiriki watahitaji kucheza
vizuri kwa kiwango cha juu katika mchezo ili kujipa nafasi ya kushinda mashindano
haya na kufanya nchi zao kujivunia. Timu nne zitakazo shiriki katika
robo fainali ya kipindi cha kwanza ni:
·
Gregory
Doamekpor na Kyei Edmond Nana, wenye umri wa miaka 21 kutoka Accra,Ghana. Hawa
walikuwa washindi katika sehemu ya kwanza ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE Ghana.
Gregory ni mwanafunzi wa Saikolojia na ndiye kichwa cha timu wakati Kyei ni
mwanafunzi wa Mahusiano ya jamii, atakuwa anachezea mpira.
· Timu
kutoka Uganda itakuwepo pia, Ibra Kawooya(30) na Alex Muyobo(31),wote mashabiki
wa Man.United, Ibra atakuwa kichwa cha timu wakati Alex atacheza uwanjani. ·
Kutoka
Cameroon watakuwa Emerand Tchouta(24) na Abdul Salam(25). Emerand atakuwa
kichwa cha timu na Abdul ataonesha uwezo wa kusakata kabumbu. Japo walifanikiwa
kuondoka na dola 1,500 tu lakini walionesha kiwango kizuri hivyo wana nafasi
kubwa ya kushinda. ·
Timu
nyingine kutoka Kenya Francis Ngigi(23) kutoka Nairobi na Kepha Kimani(25) kutoka
Thika.Timu hii ilishinda dola 3,000 katika mashindano ya GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE. Francis atakuwa kichwa cha timu wakati Kepha ataonesha kipaji chake
cha kucheza soka.
Meneja wa kinywaji cha Guinness,
Davis Kambi alisema: “Tumeona timu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali
zilishindana kufikia hatua ya robo fainali ya Pan-African- GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE na sasa tunafurahia kuona timu zetu bora katika hatua za mwisho. Kila
timu imeiwakilisha vizuri nchi yake na wamefanya vizuri katika mashindano haya
kwa kujiamini. Sasa timu zote zina nafasi ya kuthibitisha uwezo wao wa kucheza
na si kuangalia tu pale watakapo shindana ili kufikia nusu fainali.Tunasubiri
kwa hamu na kuzitakia timu zote kila la heri!”
Robo fainali ya kwanza ya
Pan-African itaoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV kwa hiyo hakikisha unaangalia na kuishangilia
timu ya taifa lako. Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa
kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.
Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
No comments:
Post a Comment