Marehemu Mzee Peter Azaria
Mbughuni, aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam amezikwa leo katika makaburi ya
Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mbughuni ameacha mke Bi. Anna Mbughuni na watoto watatu
Mhando Mbughuni, Ndojime Mbughuni na
Thabea Mbuhuni na mjukuu mmoja pamoja na wakwe zake wawili (Mke wa Mhando na
Ndojime) .
Marehemu Mbughuni alizaliwa
tarehe 25 Mei, 1950 na kufariki 9 Aprili, 2013 amezikwa na mamia ya wakazi wa
Dar es Salaam , Tanga na Morogoro ambako aliishi na kufanya kazi wakati wa uhai
wake.
Mhando Mbughuni na Thabea Mbughuni wakimfariji mama yao.
Waombolezaji wakiweka sawa sanduku lililona Mwili wa Marehemu Mbughuni kabla ya kulishuisha kaburini.
Sanduku likiteremshwa kaburini kwa mashine maalum.
Familia ya Marehemu Mbughuni...
Mhando akimfariji mama yake
Waombolezaji mbalimbali ambao ni ndugu jamaa na marafiki kutoka Dar es Salaam, Tanga na Morogoro hasa Mzumbe wakiwa makaburini.
Prof.
Joseph Kuzilwa wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe nae aliwakilisha
chuo hicho alichowahi kufanyia kazi Marehemu Mbughuni.Aliyeketi ni Mama Fatukubonye wa Mazimbu Morogoro.
Waombolezaji Makaburini wakati wa Mazishi
No comments:
Post a Comment