****** ******
BALOZI
wa china nchini Tanzania Lu Younqing ambaye yupo mkoani Ruvuma kwa
ziara ya siku tatu ameahidi kuleta wawekezaji zaidi na watalaamu wengi
katika sekta ya kilimo cha mahindi ili kulifanya zao hilo liwe la kibiashara linalozalishwa kwa njia ya kilimo cha kisasa zaidi na kuwafanya wakulima wa zao hilo kujikwamua zaidi kichumi .
Ahadi hiyo aliitoa wakati wa siku ya kwanza ya ziara
yake alipokuwa akikagua mashamba mbalimbali ya kilimo cha mahindi
ambacho kinachofanywa na wakulima wa zao hilo latika jimbo la Peramiho
mkoani Ruvuma .
Katika
ziara hiyo ya balozi Lu Younqing alitoa misaada mbalimbali kwenye
vikundi vya kijamii na wakulima vilivyopo katika jimbo la Peramiho
ikiwemo shule ya sekondari ya Namihoro iliyopo katika kijiji cha
peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Vikundi hivyo vilivyopata msaada huo ikiwemo sekondari
ya Namihoro iliyopewa shilingi milioni 10 ili kuendeleza elimu katika
shule hiyo ,kikundi cha wakina mama wajasiriamali kilipewa vyerehani
20 ili wajikwamue kiuchumi na baiskeli 20 kwa viongozi wa jumuiya ya
vijana wa CCM wa kata zote za jimbo hilo la Peramiho.
Aidha
balozi huyo kabla ya kuhitimisha ziara yake hiyo ya siku tatu
atatembelea pia mashamba ya kilimo cha kahawa yaliyopo katika wilaya ya
Mbinga mkoani Ruvuma ili kubaini changamoto zinazokabili kilimo hicho na
kuwa akielekea wilaya ya Mbinga amepita kwenye barabara ya kiwango cha
lami iliojegwa na nchi ya China kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.
Ziara
hiyo ya balozi wa China kutembelea mkoa wa Ruvuma umekuwa ni mwaliko
rasmi wa mbunge wa jimbo la Peramiho kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Jenista
Mhagama ambaye aliwataka wananchi wa jimbo hilo kutumia fursa hiyo ya
ujio wa balozi huyo kwa kufanya kazi zaidi katika kilimo kwa sababu
balozi huyo ameahidi kulifanya zao la mahindi kuwa zao la kibiashara.
Alisema
kuwa kilimo cha kisasa ndicho kinachoweza kuwakwamua zaidi kuichumi na
kuondokana na wimbi la umasikini linalowakabili pia aliwataka wananchi
kutumia fursa hiyo na misaada iliyotolewa kwao na balozi huyo kama
changamoto kwao katika kujikwamua kiuchumi na kupambana na umasikini
uliopo.
Chanzo: www.demashonews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment