April 19, 2013

KINANA AMALIZA ZIARA YA WILAYA YA GAIRO AELEKEA MVOMERO

 Wazee wa Gairo wakimpa zawadi ya silaha za jadi Ndugu Kinana kabla ya kufanya mkutano wake wa hadhara jioni ya leo kwenye uwanja wa shule msingi Gairo,wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
 Ndugu Kinana akijaribu silaha ya jadi aliyokadbidhiwa na wazee wa Gairo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Gairo,mkoa wa Morogoro kwenye mkutano wake wa ku maliza ziara yake wilayani  humo,uliofanyika uwanja wa Shule ya msingi Gairo jioni ya leo.
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Gairo,mkoa wa Morogoro kwenye mkutano wa kumaliza ziara wilayani humo,uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Gairo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wakazi wa kata ya Chakwale,wilaya ya Gairo mapema leo mchana,alipokuwa akizindua shina jipya la wakereketwa wa chama hicho.katika uzinduzi huo Kinana aliwaasa  na kuwahimiza wakazi wa eneo hilo kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kijitegemea badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu ikiwemo na suala la kuwapa ajira.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwapa kifuta jasho baadhi ya wazee-waasisi wa chama cha CCM,kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa shina jipya la kata yao ya Chakwale,Wilaya ya Gairo mapema leo mchana.Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM wako ndani ya Wilaya ya Gairo katika ziara ya kuimarisha chama cha CCM mkoani Morogoro sambamba na kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza jambo mbele ya wakazi wa Chakwale mara baada ya shina la kata hiyo kuzinduliwa mapema leo mchana,ndani ya wilaya ya Gairo.
Baadhi ya Wazee waasisi ndani ya CCM-Kata ya Chakwale wakionesha kadi zao za chama cha CCM walizonazo tangu kuanzishwa kwa chama hicho,kwenye shughuli fupi ya kuzindua shina la kata hiyo.
Kijana aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA akiwa ameinyanyua kadi ya chama chake cha awali,na kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM,akiwa kama mwanachama mpya wa chama hicho cha CCM


Baadhi ya Vijana wakiwa kwenye ajira ya kujitegemea,kama waonekanavyo pichani wakitumia mashine aina ya Trekta kupukuchua mahindi
Baadhu ya wanachama wapya waliojiunga na chama cha CCM wakionnyesha kadi zao chama,mara baada ya shina la kata ya Kibedya kufunguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana,mapema leo wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Mbunge wa Jimbo la Gairo,Mh.Shabiby akizungumza jambo na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye ndani ya kata ya Kibedya,wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Mbunge wa Jimbo la Gairo,Mh.Shabib akifafanua jambo mbele ya wakati wa kata ya Kibedya mapema leo ndani ya wilaya ya Gairo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Chakwale,wakielekea kushuhudia uzinduzi wa shina jipya la kata hiyo..
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa mmoja wa wazee wa kata ya Chakwale,Mzee YohanaChibuya.

No comments:

Post a Comment