April 30, 2013

Kamishina Jenerali Wa Jeshi La Magereza Nchini,John Casmir Minja Awatunuku Nisshani Askari 21 Wa Jeshi La Magereza Kanda Ya Kusini

Askari 21 wa jeshi la magereza kanda ya kusini, wametunukiwa nishati za heshima na kamishina jenerali wa jeshi hilo, John Casmir Minja, kwa niaba ya amiri jeshi mkuu wa majeshi nchini Rais, Dkt, Jakaya
Kikwete, katika gereza la Lilungu mjini Mtwara.

Nishati hizo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni ya utumishi uliotukuka, ya mwenge wa uhuru na ya Utumishi wa muda mrefu, ambapo nishani ya   Utumishi uliotukuka hupewa askar ambaye ametumikia kwa miaka 20 mfululizo, ya mwenge wa uhuru ni yule ambaye alizaliwa wakati nchi yetu inapata uhuru na ametumikia kwa miaka 35 mfululizo na ya Utumishi wa muda mrefu hupewa yule aliyetumikia kwa miaka 15
mfululizo.
 
Kamishna wa Magereza akikagua gwaride maalum.
Kamishina jenerali wa jeshi la magereza, John Casmir Minja akikagua gwaride la heshima kabla ya kuwatunukia askari wa jeshi hilo 21, kanda ya kusini.
Picha juu na  chini ni Kamishina jenerali wa jeshi la magereza, John Casmir Minja akiwatunuku nishani maofisa  21 wa jeshi la magereza kanda ya kusini
Maofisa  Watunukiwa wakisubiru kupata nishani zao.
Kamishina jenerali wa jeshi la magereza, John Casmir Minja akiwa na Akiwa na viongozi wa Wilaya na Mkoa.
  Kamishina jenerali akiwa na maafisa wa ngazi za juu wa jeshilo hilo katika picha ya pamoja.
Kamishina katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishani kanda ya kusini.Picha zote na Godwin Msalichuma

No comments:

Post a Comment