Wilaya 94 zimefikiwa katika zoezi la unyweshaji
dawa za Matende na Mabusha na utoaji
elimu linaloendeshwa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti magonjwa yasiyopea
kipaumbele (NTD) unaoratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dakta Mwelecele Malecela
ameyasema hayo mjini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika
Kongamano la 27 la taasisi hiyo la Sayansi la Kongamano la Pili la Afya Moja
Afrika linaloendelea mjini humo.
Dk. Malecela amesema watu milioni 14 wamenufaika
na huduma ya matibabu ya mabusha na matende katika wilaya hizo 94 ambazo zimefikiwa katika
zoezi la ugawaji dawa na tiba.
Aidha alieleza kuwa katika wilaya ya pangani
jumla ya watu mia mbili waliokuwa wanasumbuliwa na mabusha wamepatiwa tiba kwa
njia ya upasuaji na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea
na shughuli za maendeleo ya jamii yao.
Dk. Malecela amesema Programu ya kudhibiti
Metende na Mabusha imeandaa mkakati maalum wa elimu kwa umma utakaowawezesha
watanzania kupata elimu na mbinu za kuwawezesha kushiriki harakati za kitaifa
za kutokomeza magonjwa hayo nchini ambayo yameleta hofu na mashaka katika jamii
kufuatia imani potofu.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa NIMR ameitaka jamii
kushiriki katika zoezi la unyweshaji dawa kwa miaka mitano mfululizo bila kuchoka
ili kuweza kumaliza dozi na hiyvo kuweza kujikinga na maambukizi na hatimaye
kutokomeza magonjwa hayo.
Dk. Malecela amesema
Wilaya ya Tandahimba, mkoani Lindi imefanikiwa kupunguza wagonjwa wa matende na mabusha na
kufikia kiwango cha chini ya asilimia moja kutokana na jitihada za pamoja zinazoendelea za kutokomeza
magonjwa hayo chini ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza magonjwa yasiyopewa
Kipaumbele.
Pamoja
mbu wa malaria aina ya Anopheles, ugonjwa wa Matende na mabusha pia huambukizwa
kwa na mbu aina ya Culex.
Magonjwa
haya pia husababishwa na minyoo
inayoishi kwenye damu na maji damu ambayo husababisha madhara makubwa kwenye
miguu ,matiti, mikono na makende.
Mbu
aina ya Anopholes huweka mazalia yake katika maji yaliyotuama ambapo Culex
huweka mazalia yake katika maji machafu yakiwwemo yale katika mashimo ya choo
na madimbwi.
Aidha
Dk.Mwele amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa sana kwani mfuko wa rais
wa kupambana na matende na mabusha umeonyesha mafanikio makubwa na kuwezesha
watu kupata matibabu kwa njia ya upasuaji.
Wagonjwa
480 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mabusha katika mkoa wa Lindi katika mwa
huu, ambapo wagonjwa 54 kati yao wamekwishafanyiwa upasuaji huo Mwezi April
mwaka huu.
Dk. Mwele Malekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR akifungua Mjadala juu ya Utafiti wa udhibiti wa ugonjwa wa mabusha na matende kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Baadhi ya washiriki ambao ni watafiti wakifuatilia mada za mjadala huo.
Dk. Upendo Mwingira akitoa mada yake juu ya matumaini ya kutokomeza Ugonjwa wa Matende na Mabusha hasa kufuatia utafiti wake Wilayani Tandahimba.
Mmoja wa watafiti
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majidiliano hayo juu ya ugonjwa wa matende na Mabusha.
Watoa mada mbali mbali kutoka nchi za Afrika wakitoa mada zao juu ya Tathmini ya ugonjwa wa Mabusha na Matende katika nchi zao.
No comments:
Post a Comment