April 29, 2013

CRDB YAKABIDHI JENGO LA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO

 Jengo la Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ikionekana ikiwa katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya CRDB na kugharimu kiasi cha sh. milioni 50.
 Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo (kushoto) akifurahjia jambo na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kati) na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey. 
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa wameshika miche ya miti tayari kwa kuanza zoezi la upandaji miti kuzunguka katika maeneo ya hospitali ya Mkoa wa Morogoro. 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akipanda mti wa kumbukumbu baada ya uongozi wa benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro lililofanyiwa ukarabati pamoja na kuwekewa vifaa muhimu katika wodi hiyo. Jumla ya Sh. Milioni 50 zimetumika katika ukarabati huo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.


 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati), akishiriki kufanya usafi katika jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dk. Charles Kimei akishiriki katika zoezi la kufanya usafi. Hafla hiyo ilifanyika mjini Morogoro juzi. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.


 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiteta jambo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Mashishanga.


 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati) akipokea mfano wa ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati wa kukabidhi jengo la wodi ya watoto ya Hospitali ya Mkoa wa  Morogoro,  ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika mjini Morogoro juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey.


 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid  akizindua wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro.


 Kutembelea wodi ya watoto.


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akitandika kitanda baada ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto lililofanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitandika kitanda baada ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto lililofanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. 
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakiweka chandarua katika kitanda wakati walipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya uongozi wa benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi hiyo ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. Kulia aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Juma Ngasongwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
Picha ya pamoja. 

 Wafanyakazi wa benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akiingia ukumbini wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wao. 
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wadau wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na wadau wa benki hiyo katika ukumbi wa Nashera mjini Morogoro. 
 MC wa hafla hiyo akiwa kazini.
 Msanii Mrisho Mpoto wa Mjomba Band akiimba kwa hisia. Kulia ni mwimbaji wa benki hiyo, Ismail Kipira.
 Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Juma Ngasongwa ambaye kwa sasa ni mkulima wa Mpunga akiwa na wadau kataika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akikata keki na Mkurugenzi wa tawi la Morogoro,  Pendo Assey. 
 Mdau wa benki ya CRDB, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo akipata keki.
 Wateja mbalimbali wakipa keki.
 Vinywaji kama kawa.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kushoto) akiwa na maofisa wa benki hiyo.
 Muziki ulishika kasi

No comments:

Post a Comment