April 05, 2013

BARABARA YA TABATA BARAKUDA - VINGUNGUTI ILIVYO KATIKA HALI MBAYA



Hii ndio hali halisi ya Barabara ya Vingunguti-Tabata Barakuda ilivyuo sasa wakati huu wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na nchini kwa ujumla.

Wakazi wa maeneo hayo ambapo barabara hiyo inapita na watumiaji wa barabara hiyo wameimba serikali kuishughulia njia hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa wakazi walio wengi wa Tabata na Ukonga.

Barabara hiyo inakabiliwa na madimbwi mengi ya maji na tope jambo ambalo linatishia usalama wa vyombo vya usafiri na vingine vimekuwa vikizimika katika mashimo hayo.

 Mwendesha guta nae alilazimika kuikokota baada ya kunasa katika dimbwi la maji.

 Mwendesha Bodaboda akijaribu kuvuka moja ya madimbwi katika barabara hiyo.
 hawa nao walikuwa wakitafakari namna ya Pikipiki yao itakavyoweza geuka Mtumbwi.
 Hii ndio njia ilivyo.
 Serikali haina budi kutupia machobarabara hii ambayo hapo awali ilikuwa inachangamoto tu ya Daraja la Vingunguti ambalo limejengwa.
Huyu alizimika katikati ya dimbwi la maji kabla ya kupandisha mwinuko wa barakuda.

No comments:

Post a Comment