Katibu
wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib, akionyesha kadi za Chadema
ambazo vijana waliokuwa wanachama wa chama hicho waliamua kumkabidhi
papo hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano mkubwa
wa hadhara uliofanyika Aprili 15, 2013, kwenye Kijiji cha Mwaya,
Ulanga mkoani Morogoro.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa
mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea
tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama
kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC,
Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya
Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa
kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana
CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013.
Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi
kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni Nahodha wa timu
ya Nkongo, Abdallah Mazengo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Magdalena Mashinga,
alimkabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya kwenye tawi la CCM la
Mawasiliano, wilayani Ulanga,Aprili 15, 2013, akiwa katika ziara ya
kuimarisha uhai wa chama mkoani Morogoro. Kushoto ni Katibu wa NEC,
Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib na Mwenyekiti wa CCM mkoa hu,
Innocent Edward.
Wananchi
wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa
hadhara wa CCM uliofanyika Aprilki 15, 2013 kwenye Uwanja wa Mwaya,
Ulanga mkoani Morogoro.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara
katika Kijiji cha Mwaya, Ulanga, Morogoro, Aprili 15, 2013.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa
aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Abeid Mloka aliyetangaza kuhamia
CCM, wakati Kinana alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji
cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Mloka alikuwa
miongoni mwa vijana watano walioamua kuahamia CCM papo hapo.
Picha na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment