Waandishi wa
habari waliohudhuria semina ya ya upigaji picha iliyodhaminiwa na kampuni
ya simu ya Airtel jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Airtel
Money Asupya Nalingigwa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wapiga katika
semina ya upigaji picha iliyofanyika jijini Dar Es Salaam, akifuatiwa ni Afisa
uhusisano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki na Muhadhiri wa Chuo Kikuu Richard
Ndunguru.
***** ******
Kampuni ya
simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya kibebki ya Airtel Money
kwa mara ya pili imedhamini semina ya wapiga picha wanahabari inayofanyika kwa
muda wa siku mbili hapa jijini Da r Es Salaam kuanzia leo 18 hadi 19 Apili
2012.
Airtel
kupitia huduma yake ya Airtel Money imedhamini kampuni ya jijini
Dar es salaam ijulikanayo kama MP5 2011 entertainment kuandaa semina
maalum itakayowakutanisha wataalam na wapiga picha za habari wa muda mrefu
kukutana na wanahabari wapiga picha ili kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo
mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi za.
Akiongea kwa
niaba ya waandishi wapiga picha waliohudhuria semina hiyo Bw, Selemani Mpochi
mpiga picha wa muda mrefu nchini alisema “hii ni sehemu muhimu sana kwetu
wanahabari kujitengenezea utaratibu wakukaa pamoja na kutafakari mambo muhimu
ili kuendelea kufanya kazi zetu kwa ufanis.
Kwa niaba ya
wenzangu wote tunawashukuru sana Airtel kupitia huduma yao ya Airtel Money kwa
kutudhamini katika semina hii kwa mara ya pili sasa, tunashukuru sana kwa
ushirikiano wao wa kuwa tayari kutusaidia kuendeleza taaluma yetu na kuonyesha
kuwa wanatambua umuhimu wa wanahabari ncin.i
Airtel
inaendelea kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa
watanzania wengi wamenufaika kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania
wengi kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa
kupitia huduma hivyo semina hii ni njia nyingine itakayoweza kuinua kiwango cha
mapato na uelewa wa Airtel Money kwa waandishi wa habari nchin.
Zaidi ya
wapiga picha za habari wapatao 15 toka vyombo vya habari nchini wanatarajiwa
kuhudhuria semina hiyo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa msimbazi center
No comments:
Post a Comment