March 21, 2013

SERIKALI YA TANZANIA NA BODI YA UTALII YA NEPAL KUSHIRIKIANA KATIKA KUUTANGAZA UTALII KATIKA NCHI ZAO.

Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa (kulia) Kwanza ningependa kuwapongeza akinamama hawa kutoka Nepal kwa ujasiri waliouonyesha kwa kupanda mlima Kilimanjaro, na pia hilo lisingewezekana bila msaada wa Bodi ya Utalii ya Nepal hivyo tunawakaribisha sana Tanzania na tuko tayari kutangaza utalii baina ya nchi zetu hizi.

Leo tunasherehekea mafanikio ya kundi la akinadada kutoka Nepal ambao wamepanda mlima Everist lakini ili kuonyesha kwamba wanawake wakiwezeshwa wanaweza pia wamekuja kupanda Mlima Kilimanjaro. Tukio hili kwa ujumla litasaidia sana kuitangaza Tanzania katika Nyanja ya utalii ikizingatiwa kuwa waandishi kadhaa wa habari kutoka nje walikuwepo nasi tunaahidi kutoa ushirikiano.(Picha na Zainul Mzige Mo Blog)

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Utalii ya Nepal Subash Niroula akizungumza na waaandishi wa habari ambapo amesema ukweli mafanikio ya program yatatufikisha mbali katika suala zima la utalii, ikizingatia hata sisi kuna vitu na vivutio vingi vya utalii vilivyopo Tanzania tulikuwa hatuvijui hivyo naamini tutafika mbali na kufanikiwa kuvutia watalii wengi zaidi. Kwa kweli tumepata fursa nzuri kuzungumza na idara ya utalii ya Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vya kipekee miongoni mwa nchi za Kusini Mwa jangwa la sahara.

Kwa nafasi hii pia watu watapata kuifahamu Nepal, kiutalii, kiutamaduni na zaidi ya hapo kupitia ushirikiano wetu na Tanzania.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani(WFP) Bw. Richard Ragan akizungumzia shirika lake lilivyoona umuhimu wa Program hiyo na kuamua kushiriki katika kuifanikisha.
Mratibu wa Msafara wa 7 Summit Women Team Shailee Basnet kutoka Nepal akielezea uzoefu wake baada ya kupanda Mlima Kilimanjaro na Milima mingine ikiwemo milima Evarest ambapo wamekutana na mengi yakufurahisha na kuwashukuru Watanzania waliowapokea vizuri na kuwapa ushirikiano kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho.
Mratibu wa Msafara wa 7 Summit Women Team Shailee Basnet kutoka Nepal akiwaonyesha wageni waalikwa picha zinazoonyesha Hali halisi ilivyokuwa mpaka kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro wakati wa chakula cha usiku kwa ajili ya kuwapongeza wakinamama hao 10 wakiwemo 7 kutoka Nepal, 2 kutoka Tanzania na aliyekuwa mwigizaji wa tamthilia ya Isindingo maarufu kwa jina la Nandipa.
Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa (kulia) na mkewe. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Aloyce Nzuki wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa ajili ya kuwapongeza wakinamama 10 waliopanda Mlima Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani(WFP) Bw. Richard Ragan akionyesha baadhi ya picha zake wakati alipopanda katika Kilele cha Mlima Mrefu kuliko yote Duniani kwa wageni waalikwa.
7 Summit Women Team kutoka Nepal walioshiriki kupanda milima kadhaa ikwemo Mlima Kilimanjaro wakitoa shukrani kwa kumkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa (kulia) kwa mchango wake katika kufanikisha Program ya kutanga utalii nchini Nepal na Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Aloyce Nzuki akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Utalii ya Nepal Subash Niroula kwa kutambua mchango wake.
Austin Makani kutoka UNHCR akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Utalii ya Nepal Subash Niroula kwa kusaidia kuunganisha mawasiliano katika nyanja tofauti kati ya Tanzania na Nepal.
Mmoja wa wanawake kutoka Tanzania aliyeshiriki katika zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro akipongezwa kwenye hafla maalum.
7 Summit Women Team katika picha ya pamoja na timu nzima iliyofanikisha Programu hiyo.
Bodi ya Utalii ya Nepal kwa mara ya kwanza imeandaa programu ya aina yake ya kuhamasisha utalii katika bara la Afrika iliyofanyika nchini Tanzania.

Programu hii imeandaliwa kwa mtazamo wa kusherehekea safari ya kipekee iliyofanywa na Seven Summit Women Team, ambao tayari wamepanda vilele vya mlima Evarist, Mlima Kosciuszko (Australia), Mlima Elbrus (Europe) na sasa wamepanda kilele kirefu kuliko vyote Afrika cha Mlima Kilimanjaro ulioko Tanzania.

Wakati wa kuadhimisha mafanikio hayo ya kihistoria ya Seven Summit Women Team, Bodi ya Utalii ya Nepal imechukua fursa hiyo kutangaza na kuhamasisha utalii nchini Nepal kama moja ya vivutio bora duniani.

Bodi ya Utalii ya Nepal imekutana na waendeshaji shughuli za kitalii wa Tanzania ili kuiwezesha Nepal kuwa moja ya vivutio vya utalii na pia kujenga uhusiano na Tanzania ili kwa pamoja kuhamasisha nchi hizo mbili kuwa vivutio vya kipekee.

Ushirikiano huu kati ya Serikali ya Nepal kupitia Bodi ya Utalii na Serikali ya Tanzania umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania kwa kiasi kikubwa inatangaza utalii na hivyo kutatoa mwanya sahihi wa kuwa na mawasiliano na kubadilishana taarifa miongoni mwa wahusika wa utalii kwa pande zote za Nepal na Tanzania.

No comments:

Post a Comment