March 21, 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA DARAJA LA SUKA GOLANI KIMARA SUKA JIJINI DAR LEO

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo.Kushoto anayeangalia ni mbunge wa Ubungo John Mnyika.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Madabida,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik,Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda na kushoto ni Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika.


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea  Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Yusuf Mwenda  na  mbunge wa Ubungo John Mnyika.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waishio eneo la Golani  Kimara Suka muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani.
 Wananchi wa vyama mbalimbali vya Siasa wakishangilia wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwahutubia muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo mchana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ubungo John Mnyika wakati alipokwenda kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo

No comments:

Post a Comment