Mshambuliaji
wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu akiwatoka
Golikipa na Beki wa Timu ya Taifa ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania
tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini
Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es
Salaam.Taifa Stars imeshinda Bao 3 - 1,mabao yaliyotiwa kimiani na
Mshambuliaji Machachari,Mbwana Samatha na Thomas Ulimwengu.
*********
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ wanaosakata soka la Kulipwa nchini Kongo DRC, katika timu ya TP Mazembe,
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu leo wamewathibitishia kile ambacho
waliwaahidi watanzania siku kadhaa zilizopita wakati walipowasili nchini
kujiunga na kambi ya timu ya taifa.
Samatta na Ulimwengu waliwaahidi watanzania
ushindi dhidi ya timu ya Morocco katika mchezo wa kundi C kuwabnia kufuzu
fainali za kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Alikuwa ni Thomas Ulimwengu aliyewanyanyua
mashabiki na wapenzi wa Soka Tanzania baada ya kuipatia Taifa Stars bao la
kuongoza katika dakika ya 46 ya kipindi cha pili.
Dakika ishiri baadae Mbwana Samatta alimalizia
kazi nzuri iliyofanywa na Thomas Ulimwengu ambaye nae alipokea pasi toka kwa
Athuman Idd ‘Chuji’ bao lililofungwa dakika ya 66.
Alikuwa ni Mbwana Samatta tena aliyewanyanyua
watanzania katika viti baada ya kupachika msumari wa mwisho mnamo dakika ya 86
akimalizia pasi ya Ulimwengu.
Morocco walipata goli lao la kufutia machozi
katika dakika ya 90 +4 kupitia kwa Yousef Elarabi.
Kwa matokeo hayo, Stars inaendelea kushika
nafasi ya pili katika Kundi C kwa pointi zake sita, nyuma ya Ivory Coast
inayoongoza kwa pointi zake saba, baada ya jana kushinda 3-0 dhidi ya Gambia.
Stars sasa inakabiliwa na kibarua kigumu kwa mechi mbili za ugenini dhidi ya Morocco na Gambia huku Ivory Coast wakisubiriwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Viosi vya leo ni
Taifa Stars:- Juma Kaseja (Nahodha), Erasto
Nyoni, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Salum Abubakar ‘Sure Boy’,
Mrisho Ngassa/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk 63, Frank Domayo, Mbwana Samatta/Jahn
Bocco dk 91, Mwinyi Kazimoto/Thomas Ulimwengu dk46 na Amri Kiemba.
Morocco:- Nadir Lamyaghri, Younes Belakhadr,
Abdelilah Hafidi/Nuredenne Amrabat, Zakarya Bergdich, Abderrahim Achchakir,
Younes Hammal, Abdelaziz Barrada, Issam Eladoua, Kamal Chafni, Chahir
Belghazouani/Youssef El Arabi na Hamza Abourazouk.
No comments:
Post a Comment