March 27, 2013

LOWASA AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI MAZISHI YA NYITI ARUSHA



Mh Lowassa akiongoza viongozi kwenda kwenda kuweka udongo kaburini,nyuma yake ni Waziri wa mambo ya nje Mh Bernard Membe.

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ameongoza maelfu ya Wakati wa mji wa Arusha na mikoa ya jirani katika mazishi ya mfanyabiashara na Kanda maarufu wa CCM Mkoani Arusha Henry Nyiti,nyumbani kwake Tengeru Arusha.

Nyiti alifariki ghafla wiki iliyopita akiwa katika mgodi wake wa madini,Mahenge Mkoani Morogoro.

Wengine waliyoudhuria Ni pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe,Naibu Waziri wa maliasili na utaalii Lazaro Nyalandu,mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr Reginald Mengi,Mkuu wa mkoa wa Arusha, mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Ridhiwani Kikwete.
 
 Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa pia alikwenda kutoa pole katika msiba wa Moja wa wazee maarufu eneo la Mto wa Mbu, mzee Athman.
Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe akiweka udongo
Mh Lowassa akisalimiana na Mh Mbowe


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akiweka shada la maua

No comments:

Post a Comment