Wakati Mamlaka ya
Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) juzi iliamua kuingia rasmi katika Mfumo wa
Mawasiliano ya Televisheni na Redio kwa kurushwa katika mfumo wa kisasa wa
Dijitali kutoka ule mfumo wa Analojia, Shirika la Usambazaji Umeme TANESCO nao
wameamua kuingia katika Mfumo wa Dijitali kwa staili ya kupandisha nguzo ya
Umeme katika mti halisi ambao bado unamea kama jinsi taswira hizi
zinavyoonesha. Hii ni Huko Mkoani Ruvuma, na TANESCO mkoani humo wameamua
kutumia njia hii kurahisisha usambazaji umeme.
Pia baadhi ya wananchi
wanahoji au shirika limeamua kufanya hivi baada ya udhibiti wa Nguzo hewa
kutoka Afrika Kusini kufanyika? Ama ndo teknolojia yao Mpya 2013.
Jionee jinsi Tanesco walivo nateknolojia ya kisasa
Kweli huu ni mwaka mpya
Mambo hayo
Jiulize kwa hali kama hii Tanesco wako juu kwa mfumo huu au wanajaribu nao mfumo wao mpya:SOURCE:Demashonews Blog
No comments:
Post a Comment