JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI NA MICHEZO
Waziri wa
Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewatumia
salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo
cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe
02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa
iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na
Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za
kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia
ya filamu hapa nchini.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa
tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.
“Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya
kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika
tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt.
Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na
watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa
Mwenyezi Mungu.
Juma
Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza
kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na
baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja na Revenge ya Kampuni ya
RJ .
Mwaka
2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya
kwanza iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious
ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY
Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni
Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero
Seven Seven).nk.
Sajuki
alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye
majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na
Uongozaji wa filamu.
Sajuki
alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo
alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu
walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata
matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo
lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza
kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya
utengenezaji.
Aidha
hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe
02/01/2013.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen.
Imetolewa na:
Mkurugenzi
Idara ya Habari(MAELEZO).
Dar es Salaam.
2 Januari 2013
**********
Yah: Salaam za Rambirambi
Baraza
la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa
tasnia ya filamu nchini Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki.
“
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha
Sajuki ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo
aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.”
Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia
moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Tunaomba
mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko
pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo,
tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.
Imetolewa
na
Ghonche Materego
Katibu
Mtendaji
Baraza
la Sanaa la taifa.
No comments:
Post a Comment