WAKAZI wa Jiji la Dar es
Salaam jana Januari 1, 2013 walifika kwa Wingi katika Fukwe ya bahari ya Hindi
eneo la Coco Beach kwaajili ya kupunga upepo na kuogelea ikiwa ni sehemu yao ya
maadhimisho ya Mwaka mpya. Wakazi hao ambao ni watu wazima na watoto walifurika
kwa wingi katika eneo hilo na kufurahia siku kuu hiyo ya mwaka mpya.
Sehemu ya Umati wa watu ukiwa katika Fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Coco.
Wakazi wa Dar es Salaam wakiwa wamepumzika katika eneo hilo la Ufukwe wa Coco
Watu wengi walifika kwaajili ya Kuogelea na hakika licha ya mawimbi makubwa lakini walimudu vyema kuogelea na kuifurahia siku kuu ya Mwaka Mpya.
No comments:
Post a Comment