Waziri wa Jinsia wa Rwanda, Aloysia
Inyumba amefariki, jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akiwa bado kijana aliyehitimu kutoka
Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, Inyumba alishiriki kikamilifu katika
kuasisi chama cha Rwanda Patriotic Front (RPF) mnamo mwaka 1987.
Katika Harakati hizo akawa Kamishna wa
Fedha wakati wa mapinduzi ya RPF ambapo alipata uwezo wa kuweza kukusanya na
kutunza fedha kwaajili ya Mfuko huo wa Mageuzi.
Inyumba alijizolea umaarufu mkubwa
wakati wa kufanya manunuzi ya sare mpya za jeshi la RPF kutoka Ujerumani
Mshariki maarufu kama Mukotanyi .
Inyumba alishika wadhifa huo wa Waziri
wa Jinsia tangu baada ya vita 1994, na baade kuwa mbunge kwa miaka 8 na kurudi
tena katika baraza la Mawaziri.
Wakati wa kuzanzishwa kwa RPF akiwa
pamoja na marehemu Meja Peter Bayingana , alifanya kazi kubwa ya kumshawishi
Kanali Alex Kanyarengwe kujiunga nao.
Marehemu Inyumba atakumbukwa kuwa
alisafiri hadi Tanzania kufuta Kanyarengwe ambaye baade alikuja kuwa Mwenyekiti
wa RPF, kufutia kifo cha Generali Fred Rwigyema.
Hadi mauti yanamfika , Inyumba alikuwa
ni mtu muhimu sana kwa Rais Paul Kagame kwani alikuwa ni mtu mwenye ushawishi
mkubwa katika siasa.
Kifo cha Inyumba si pigo tu kwa RPF
lakini pia ni pigo kwa wana Rwanda wote.
Inyumba alikuwa akiheshimiwa sana katika uwanja wa siasa hata kwa wale walio
poteza imani zao kwa Kagame kama vile Generali Faustin Kayumba Nyamwasa.
No comments:
Post a Comment