December 17, 2012

WANAWAKE WAKIRI KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE: UTAFITI

Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi, kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa NIMR. 
***
BAADHI ya wanawake kutoka katika Wilaya za  Kinondoni, Tanga, Makete na Siha, wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile.

Hayo yalielezwa na Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) wakati akiwasilisha utafiti uliofanywa na watafiti wa NIMR juu ya ufanyaji Ngono kinyume na maumbile katika kueneza maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini na kuwasilishwa mbele ya Wanahabari na Watafiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

“ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao wal;ihusishwa katika utafiti huo,” alisema Mtafiri Irine.

Aidha alisema wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambayo ni sawa na 26.5%  huku 76.4% ya waliohojiwa walidai kufanhamu njia hiyo ya kufanya mapenzi.

Wilayani Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbe na wanaume kuwafanyia wanawake kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.

Wanaume waliohojiwa katika utafiti huo wamedai wao wanafanya kwa mtindo huo kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ikiwa ni hafifu kwani wakitumia mipira wamedai kupunguza raha wanayo ipata.

Wanawake pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana kuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo likichukua nafasi.

Watafiti hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana.

Aidha imedaiwa kuwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto, jambo ambalo limekuwa likileta tabu kwa wahudumu wa Afya hasa wakunga ambao ni wachache mahospitalini kutumia muda mrefu kumhudumia mjazito mmoja huku wengine wakiendelea kuteseka wodini wakati wa kujifungua.

Watafiti hao wameshauri elimu zaidi ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na njia salama za kujamiiana kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya kujamiiana kinyume na maumbile kuwa haiambukizi virusi vya Ukimwi.
 
Watafiti walioshiriki katika utafiti huo ni pamoja na Akili kalinga, Elizabeth  H Shayo,  Irene Mremi , Godlisten materu, Stella Kilima, Gibson Kagaruki, Anjela  Shija, Judith Msovela, Dk. Leornad Mboera, Dk.Julius Massaga, Kesheni Senkoro na Basiliana Emid wote kutoka NIMR.

9 comments:

  1. Irene hongera kwa kuwasilisha matokeo ya utafiti kuhusu ngono kinyume na maumbile ya wanawake







    ReplyDelete
  2. Irene ipo hoja kwamba wanawake wanafanya hivyo ili kupata starehe na kuongeza kipato Hii hamkuiona?

    ReplyDelete
  3. jamani huu mchezo sio mzuri kabisa inabidi tumrudie mungu kwani kwa matukio haya ni dalili za mwisho wa dunia.

    ReplyDelete
  4. kuhalalisha ngonokinyume cha maumbile kwa kigezo cha kuongeza kipato ni kupotosha ukweli.Na ukweli ukifichika hata njia za kukabiliana na tatizo hazitokuwa sahihi. Wanawake wengi either huomba au hukubali kufanyiwa hivo kwa sababu ya starehe tu, pamoja na sababu nyingine. Wliokuambia ni kuongeza kipatyo walikuficha ukwelidada irene.

    ReplyDelete
  5. Ningependa kkujua kama ngono aina hii ambayo inaitwa kinyume na maumbile inahusisha pia ngono baina ya jinsia moja (inajulikana kama kulawitiana/kusagana), uu ni kwa wanawake na wanaume tu?

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli hii tabia ya kufanya ngono kinyume na maumbile ni kosa kubwa sana kwa mwenyezi mungu na hata kwa afya ya binaadamu and then kama weweni mwanmke alafu unafanya mambo kam hayo ya ya kufanya ngono kinyume na maumbile ukija pata mimba na wakati wa kujifungua unaweza kupoteza maisha yako au mtoto.ushauri wanawake tusidanganyane kufanya hivyo,kwanza sio sababu ya kuzuia maambukizi ya ukimwi,ukimwikama ukimwi unaweza kupata kama vile wewe unaefanyiwa una mchubuko na mwenzi wako ana mchubuko basi nirahisi kupata ugonjwa.Na kufanyiwa tendo kinyume na maumbile ni kudhalilishana.akupendae akufanyii hilo tendo baya.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2013

    Utafiti haujajitosheleza zaidi ya kudhalilisha wanawake na kuonyesha ubaguzi na kutusi jamii za watu wa mwambao.Haingii akilini wanawake 44 wanaofanya kitendo hicho toka wilaya hizo nne kuwakilisha kuwa tatizo la kitaifa na kwa makusudi mazima hukwenda mbali kimaelezo zaidi ya kueleza wilaya ya Tanga kuwa kinara dhidi ya makete.Mbona hukueleza tafiti za wilaya nyengine ulizo zieleza kama Kindondoni na Siha.Kuhusu ushirikina si kweli ila kwa mchezo huo upo na umeenea kila kona ya dunia na unao washika dau wao ambao ni Marekani na mataifa ya magharibi na ndio hao hao wafadhili wenu wa miradi ya ukimwi.Je! watafiti mtuambie mna ajenda ya siri ili kuwaridhisha wafadhili wenu ili kuwaletea mapesa zaidi ya kuwa wezesha mashoga na wasagaji?.
    Ipo siku ukweli tuta ujua maana majina ya watafiti yana elemea upande mmoja wa dini na shaka yangu ipo hapo

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2013

    Acha ukweli usemwe ili tabia mbaya zikome, hii si fitina ni kweli tupu, duniani kote kuna uchafu huu, ila kuna sehemu , watu na namna zimedi. Mimi ni Mdigo asilia na wala sipingi, hili tendo lipo sana Tanga .

    ReplyDelete
  9. hii hali ipo wanawake wanaweza kushawishiwa au kumshawishi mwanaume, hii tabia imekidhiri sana sehemu za mwambao wa pwani ya Africa Mashariki. Ila awe mwanaume au Mwanamke ni ujinga mtupu na moto unawasubilia

    ReplyDelete