December 17, 2012

BWANA HARUSI ANUSURIKA KIFO SIKU MOJA KABLA YA NDOA YAKE

Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth  Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya. Bwana harusi anaonekana na majeraha baada ya kunusurika kifo katika ajali ya pikipiki na gari usiku wa kuamkia Jumapili ambayo alifunga ndoa.
Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100  Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia jumamosi mida ya saa sita nanusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndiyo ajali hiyo ikatokea maeneo ya mafiati mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo 
Hii ndiyo hali halisi iliyotokea siku hiyo ya ajali mbeya yetu tulifika usiku huo eneo la tukio na kukuta tayari majeruhi wametolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa Mbeya ndipo jana tukaamua kufuatilia majeruhi hao na kukuta kuwa Emmanueli ameruhusiwa kwa muda akafunge ndoa kwani jana ilikuwa siku ya yeye kuoa ndipo tukaenda kufuatilia harusi hiyo  katika kanisa la agape 
Bwana harusi Emmanueli na mpambe wake Frank wakiingia kanisani
Hakika ni furaha hapa bwana harusi anamtambua mkewe kwa kumfunua shela kabla ya ndoa kufungwa
Sasa bana na bibi harusi wanaingia kanisani tayari kwa ibada ya ndoa
Mchungaji Emmanuel Mwasota toka E.A.G.T toka DSM ndiyo aliyofungisha ndoa hiyo
Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete  huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea
Hapa wakipata mibaraka ya ndoa kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo la AGAPE
Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu jina la bwana libarikiwe
Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota

Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa
Maharusi wakiwa na familia na wazazi wao
Sherehe fupi ya kuwapongeza maharusi ilifanyika katika bustani ya ccm jijini mbeya
Ndugu jamaa na marafiki walihudhuria sherehe hiyo ingawa maharusi hawakuweza fika kwenye sherehe hiyo kutokana hali yake haikuwa nzuri alihitaji kupumzika na kurejea tena hospitali kuendelea na matibabu
Picha na Gwasa wa Mbeya yetu

1 comment:

  1. Binafsi kupitia hili tukio nimezidi kumuona Mungu, huyo Bwana arusi anakila sababu ya kumshangilia Mungu kwa sauti kubwa. Nawaombea maisha marefu na yenye furaha na amani tele.Nimempenda bibi arusi anaonyesha matumaini sana na upendo wa kweli kwa mumewe.

    ReplyDelete