December 08, 2012

WAMA watoa vitanda 80 kwa hospitali ya Muhimbili

Mwenyekiti wa Wama mama Salma Kikwete akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vitanda 80 kwa uongozi wa Hospitali ya Muhimbili leo, kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Mama Salma Kikwete akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi vitanda 80 katika hospitali ya Muhimbili leo (kushoto) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela akimshukuru mama Salma Kikwete mara baada ya kupokea msaada wa vitanda hivyo leo.
Baadhi ya Mganga na wauguzi wa hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo.
Mama Salma Kikwete akiongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk. Marina Njelekela kushoto wakati akielekea wodini kuwatembelea wagonjwa, kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi.
Mama Salma Kikwete akimjulia hali Anna Razalo kutoka Nyegezi Mwanza mmoja wa wagonjwa wa moyo aliyelazwa hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment