December 18, 2012

UNIQUE MODELS WAANZA MAZOEZI LAMADA


Washiriki wanaowania taji la mwanamitindo mwenye sifa za kipekee Unique model 2012 wanatarajiwa kuanza mazoezi ya miondoko ya kimaonyesho alhamisi hii katika hoteli ya Lamada iliyopo jijini Dar .Jumla ya washiriki kumi na mbili wataanza mazoezi hayo kwa nia ya kujifua kimazoezi ya kutembea miondoko ya kimaonyesho na dansi ili kuukabili mchuano mkali uliopo baina ya washiriki hao.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi mratibu wa shindano hilo Bw. Methuselah Magese amesema kuwa washiriki wapo katika hali ya ushindani sana na mwaka huu namshukuru mungu wamejitokeza wanamitindo wengi wenye sifa ukilinganisha na mwaka 2010 hii inaonesha kiwango cha ubora wa shindano kinapanda juu.

Magese aliyataja majina ya washiriki hao ni Janecy Maluli,Judith Sangu,Vestina Charles,Catherine Masumbigana,Darling Godfrey,Amina Ayoub,Elizabeth Pertty,Lulu Mramba ,Sadory Kendra,Elizabeth Borniface na Zeenarth Habib,Mwalimu wa dansi ya washiriki Denis Lucas amejiandaa vyakutosha kuhakikisha kuwa washiriki hao wanatoa burudani ya dansi amabayo haijawahi kutokea ambapo watu watapata mengi ya kukonga nyoyo zao kwa kiingilio cha elfu kumi na tano tu.

Mwalimu wa miondoko atakuwa mwanamitindo mwenye uzoefu na majukwaa ya mitindo nchini Tanzania ambae ametajwa kwa jina la Wancy Nells ambae amejipanga kuwanoa vema wanamitindo hao tayari kwa fainali.

Fainali za Unique model 2012 katika kumtafuta unique model of the year 2012 zifanyika tarehe 28 mwezi huu katika ukumbi wa maraha New Maisha club uliopo oysterbay jijini Dar.
 
Shindano hili limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general Traders,sophanaa investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie blog,Lmada Apartments & Hotel,mtaa kwa mtaa blog,Fabak fashins,Genessis health center na Yung don Records,Paka wear,Mtoko Design,Dina ismail blog na Unique Entertainment Blog.

No comments:

Post a Comment