Timu za Soka za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazoshiriki michuano ya mwaka huu ya Tusker Cecafa Challenge huko Uganda zimetimnga nusu fainali za michuano hiyo baa da ya kuzitoa mashindano timu za Rwanda na Burundi.
Wawakilishi hao ni Tanzania
bara Kilimanjaro Stars na Zanzibar ‘Zanzibar
Heroes’ zimefuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya Tusker Challenge
Cup baada ya kuwatoa vigogo hao katika hatua ya Robo fainali.
Kwa matokeo hayo ya timu hizo ambazo Kilimanjaro Stars iliibwaga
Rwanda 2-0 katika robo fainali ya kwanza na Zanzibar Heroes ikaitoa Burundi kwa
mikwaju ya Peanti 6-5 zinaweza kukutana katika fainali endapo zitafanikiwa kuwatoa washindi wa michezo ya kesho.
Robo fainali za kesho zitawakutanisha Kenya na Malawi na mchezo mwingine ni kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia.
Robo fainali za kesho zitawakutanisha Kenya na Malawi na mchezo mwingine ni kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia.
Wachezaji wa timu ya Zanzibar
Heroes na Burundi wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya pili ya
michuano ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo
Lugogo nchini Uganda leo.
Kiungo mchezeshaji wa
Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Mwinyi
Kazimoto akizuiwa na beki wa Rwanda, Ismail Nshutiyamagara wakati wa mchezo wa
Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika
Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda leo.
Kikosi cha Zanzibar Heroes
kilichopambana na Burundi katika mchezo wa Robo Fainali ya Pili ya michuano ya Tusker
Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda leo.Kikosi hichi kimeitoa Burundi kwa magoli 6-5.
Wachezaji wa Kilimanjaro
Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakitoka Uwanjani
baada ya kipindi cha kwanza kumalizika katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza
ya michuano ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo
Lugogo nchini Uganda
Kipa wa Rwanda aliyelala
chini akijitahidi kuokoa goli lililofungwa na Amri Kiemba baada ya kazi nzuri
iliyofanywa na Mwinyi Kazimoto ya kuwapita mabeki wa timu ya Rwanda
Mshambuliaji wa timu ya
Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Mrisho
Ngasa aliyelala chini na wachezaji wenzake wakishangilia kwa staili ya aina
yake baada ya kuwafunga Rwanda 2-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya
michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo
nchini Uganda
Mashabiki wa Kilimanjaro
Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wakishangilia wakati
wa mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michunao ya Tusker Cecafa Challenge
dhidi Rwanda uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda.
Kilimanjaro Stars ilishinda 2-0
No comments:
Post a Comment