Shindano la Maisha Plus limefikia tamati huku mwana dada Bereniki
Kimiro akiibuka mshindi na kujinyakulia Shilingi Milioni 20 za Kitanzania
kibindoni.
Nafasi ya pili katika shindano hilo lililo waweka vijana katika
kambini ni Venance Mushi amejishindia Tshs. Million 6 huku nafasi mshindi wa
Tatu ni Justine Bayo, amejishindia Tshs. Million 4.
Mara baada ya kutangazwa mshindi, Mshindi wa Maisha Plus 2012, Beneriki alimshuukuru Mungu kwa ushindi, na kusema kuwa ‘yeye si kitu kwa wenzake, hilo ni zali tu’..
Aidha amemshukuru baba yake mzazi kwa kumshauri kusali,a mewashukuru
pia wapenzi watazamaji kwa kumpiga kura, ameahidi kuendeleza kile alichokianza
kijijini na kuitendea haki nchi yake..
Bereniki amemshukuru babu wa Kijijini, Brother Masoud na Crew nzima
ya Maisha Plus.. Amemshukuru pia mwanae Kelvin (6yrs) kwa kuvumilia kipindi
chote bila kuongea na mama.
Amesema Mungu amejibu maombi yake kwani ukipiga goti, maombi yako
yatajibiwa.
No comments:
Post a Comment