Timu ya
soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, (Taswa FC) ni miongoni
mwa timu nane zitakazoshiriki katika bonanza maalum la kuadhimisha miaka
51 ya Uhuru wa Tanzania (Uhuru Dar Corporate Bonanza) lililopangwa
kufanyika Desemba 9 kwenye uwanja wa Gymkana.
Mwenyekiti
wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wamepokea mwaliko kutoka kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vannedrick (T) Limited, Fredrick Mwakalebela
kuhusiana na ushiriki wa timu katika bonanza hilo na wao wamethibitisha.
Majuto
alisema kuwa kampuni ya Vannedrick (T) Limited ndiyo imeandaa bonanza
hilo na kudhaminiwa na benki ya NMB na wachezaji wake kwa sasa wapo
katika maandalizi ya kina ili kutwaa ubingwa. Bonanza hilo litaanza saa
2.00 asubuhi.
Alisema
kuwa timu nyingine ambazo zitashiriki katika bonanza hilo ni Barrick,
NMB, Dstv na Radio Times ambazo zipo katika kundi A na Taswa FC pamoja
na Jubilee, Azam Group na wenyeji, Gymkhana wapo katika kundi B.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Vannedrick (T) Limited, Mwakalebela alisema kuwa
timu hizo zitachuano kwa mtindo wa Ligi na timu mbili katika kila kundi
zitafuzu hatua ya nusu fainali na baadaye fainali.
Alisema
kuwa pia kutakuwa na zawadi za mshindi wa tatu mbali ya mshindi wa
kwanza na wa pili. ”Lengo ni kuwaweka pamoja wadau wa michezo ambapo
mbali ya kuadhimisha miaka 51, tutatumia fursa hiyo kujadilia masuala
mbaali mbali ya michezo, matatizo, mafanikio na nini kifanyike,” alisema
Mwakalebela.
No comments:
Post a Comment