December 12, 2012

TANGAZO LA MSIBA

Bwana Onesmo Timothy Nathan Mroki wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam, anasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wake mpendwa Digna Onesmo, kilichotokea Usiku wa Kuamkia leo, Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mipango ya Mazishi inafanyika Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Mzee Kaluse na mazishi yanataraji kufanyika leo jijini Dar es Salaam.

Habari ziwafikie, Bibi wa Marehemu, Mary Nathan wa Kinyenze, Morogoro, Baba Mkubwa wa Marehemu, Lloyd Atenaka wa Kibaha Block B, Familia yote ya Ukoo wa Mroki na Kajiru popte pale walipo, Ndugu Jamaa na Marafiki.

No comments:

Post a Comment