MAGAZETI
mengi ya leo katika ukurasa wake wa mbele licha ya kuwa na habari zaidi ya moja
iliyopewa uzito wa kuuzia gazeti husika lakini pia kuna habari iliyopewa kichwa
‘OFISA WA TAKUKURU AMUUA MWENZAKE KWA RISASI’.
Habari
hiyo inamhusu Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Bhoke Ryoba, aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na ofisa mwenzake
wakati wakisherekea ufukweni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.
Father
Kidevu Blog , baada ya kupitia habari hizo katika magazeti kadhaa lakini
ilikutana na mkanganyiko juu ya habari hizo hasa kufuatia kuwapo kwa kauli
mbili tofauti juu ya aliyehusika kumuua Ryoba.
Ingawaje
magazeti Mengi yamemnukuu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke. Engelbet Kiondo,
na kusema bayana kuwa Ryoba alipigwa
risasi na ofisa mwenzake, Mussa John (34), mkazi wa Mabibo, jijini Dar es
Salaam.
Pia
baadhi ya magazeti yalinukuu taarifa ya Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dkt. Edward
Hoseah, iliyosema wazi kuwa Ryoba alifariki juzi jijini Dar es Salaam baada ya
kupigwa risaasi.
Sehemu
ya nukuu katika gazeti la Nipashe ilisema hivi, “Tumekuwa tukipokea simu nyingi
kutoka kwa watu wakihitaji kufahamu ukweli wa tukio la kupigwa risasi kwa
mtumishi Bhoke Ryoba, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, anapenda
kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hili kwamba ni kweli alifariki dunia Jumamosi
(juzi) usiku baada ya kupigwa risasi,” ilieleza kwa kifupi taarifa hiyo.
Hata
hivyo, taarifa ya Takukuru haikueleza chanzo cha mtumishi huyo kupigwa risasi
wala eneo lilipotokea tukio hilo, lakini iliongeza kuwa uchunguzi kuhusu chanzo
cha tukio hilo bado unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi.
Father Kidevu Blog, imekumbwa na wasiwasi juu ya utoaji wa taarifa hizi hasa kutoka Ofisi Husika ambayo Marehemu alikuwa akifanyia kazi. Hofu hii ni kwanini TAKUKURU itoe taarifa zinaoelea zisiszo za kiuchunguzi kama ofisi yao ilivyo ama kwakuwa wao hawachunguzi mauaji?
Lakini
kama hilo haliwahusi Dkt. Hoseah alikuwa pia anauwezo mkubwa sana wa
kuwasiliana na Jeshi la Polisi likampa taarifa za awali juu ya mauaji hayo
yalivyo tokea ili aitumie taarifa hiyo kutoa ufafanuzi kwa Umma kupitia vyombo
vya habari.
Gazeti
la Mwananchi mbali na kuandika habari hiyo kwa kutumia Taarifa ya Mkurugenzi wa
TAKUKURU, lakini pia waliongea na Ofisa habari wa Takukuru Doreen Kapwani na
kutoa ufafanuzi zaidi juu ya tukio hilo na kuzidi kujiweka wazi kwa tasisi hiyo
nyeti kuwa haikuwasiliana na Polisi ama walikuwa wanataka kuepusha kikombe
hicho cha kuipa jamii taarifa sahihi na za ukweli.
Kapwani,
aliwafafanulia Gzeti la Mwananchi kuwa ofisa huyo mchunguzi alifikwa na umauti
wakati anajumuika na marafiki zake katika moja ya tafrija iliyokuwa ikifanyika
katika eneo la Kigamboni.
Alisema akiwa katika hafla hiyo, ghalfa walitokea watu
wasiojulikana na kumiminia risasi hadi kufa.
Gazeti la Mwananchi lilimemnukuu Kapwani “Hawa watu
walimvamia Ryoba aliyekuwa kwenye sherehe moja na kumshambulia kwa risasi na
kisha wakatokomea kusikojulikana,” alisema na kuongeza:
“Watu hao hawakutambulika kwa kuwa baada ya kutekeleza
azma hiyo walitoweka haraka na kutokomea.”
Polisi
wao kupitia Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke. Engelbet Kiondo ilisema kuwa
tukio hilo lilitokea katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Southern Beach saa 1:30
usiku wakati watumishi wa Takukuru walipokwenda kuburudika.
Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo, wakati watumishi hao wakiburudika, ndipo mmoja wao, Mussa John, alipochukua bastola yake na kuanza kupiga risasi hewani.
Alifafanua moja kati ya risasi hizo, ilimpiga Ryoba na kumsababishia majeraha kifuani.
Baada ya kujeruhiwa, Ryoba alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu, lakini alifariki dunia usiku wa kuamkia jana wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo, John alikwenda kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Chang’ombe na anaendelea kushikiliwa.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Ahmed Msangi, na maafisa wengine wa polisi walikwenda eneo la tukio.
Kamanda Kiondo alisema katika mahojiano na polisi, John alisema kuwa alimpiga risasi marehemu kwa bahati mbaya.
Kamanda huyo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Father
Kidevu Blog ilidhani kuwa vyombo hivi viwili hasa TAKUKURU ingefanya
mawasiliano kwanza na Polisi ili kupata taarifa kamili ya tukuo hilo namna
ilivyotokea hadi kufa kwa mtumishi wake kabla ya kutoa taarifa zinaolea.
Ona
sasa TAKUKURU wanauambia Umma kupitia vyombo vya Habari kuwa Ryoba kauwawa na
watu wasio julikana ilhali Polisi wanasema wazi anaedaiwa kumuua Rhoba ni John
na amejisalimisha mwenyewe katika kituo kimoja wapo cha Polisi jijini Dar es
Salaam kwa usalama zaidi.
0 comments:
Post a Comment