December 08, 2012

MKURUGENZI MKUU WA EABC AKUTANA NA WANAHABARI WA EAC KATIKA MAFUNZO

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja. Mafunzo hayo yanahusisha wanaandishi wa habari kutoka nchi zote wanachama wa EAC, na kufanyika Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja. Wengine pichani ni washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu wa baraza la Asasi za Kijamii la Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Martin Mwodha, akizungumza katika mafunzo hayo juu ya ushiri wa Asasi za kiraia katika ulelimishaji na ufikishaji wa elimu ya Soko la Pamoja la EAC.
Mchambuzi wa Siasa za Afrika ambaye pia ni Mwanahabari Mkongwe nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu akitoa mada katika mafunzo hayo leo.
Dawati la ufundi nalo wakati wote lilikuwa katika wakati mgumu wakuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Kutoka kushotoni Aline Ellermann, Elizabeth Wanyoike na Hussein Karim wote kutoka ofisi ya GIZ ambao ndio wawezeshaji mafunzo hayo yaliyoandaliwa pamoja na AC
Kuna wakati mambo yanaonekana hayaendi na hapa anaonekana Elizabeth Wanyoike (kulia) akikuna kichwa) huku Aline Ellermann akiendelea na kazi.
Fiona Mbabazi kutoka Rwanda akimshukuru Ofisa mtendaji wa EABC, Andrew Kaggwa kwa maelezo juu ya Baraza hilo.Kati ni Jenerali Ulimwengu na Aline Ellermann.
Bizimana Jean-Marie akitoa zawadi kwa Dk. Martin Mwadha wa Asasi za Kiraia za EAC, wengine pichani kutoka kushoto ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ, Balozi  Jeremy Ndayiziga, Andrew Kaagwa na Jenerali Ulimwengu

No comments:

Post a Comment