Warembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari leo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Rena Event Limited Bw Rena Calist akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Seaescape iliyoko Mbezi Afrikana jijini Dar es salaam wakati akizungumzia matayarisho ya mwisho kabla ya shindano la Miss East Africa linalotarajiwa kufanyika kesho Desema 21 kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.
Katika shindano hilo wanashiriki warembo kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na na baadhi ya nchi jirani na ukanda h ambapo mshindi wa shindano hilo anatarajiwa kujinyakulia zawadi zenye thamani ya dola za Kimarekani elfu thelathini 30,000.
Kushoto ni Guetano Kagwa ambaye atakuwa MC wa shindano hilo na kulia ni Serge Nkurunzinza Mwakilishi wa Miss East Africa nchini Burundi .
Guetano Kagwa ambaye ni MCwa shindano hilo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kulia ni Rena Calist Mkurugenzi wa Miss East Africa.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Mpiga picha wa Clouds TV Bw. Katunda akiwa katika picha ya pamoja na warembo hao, Katunda amekuwa na warembo hao kwa muda sasa toka waingie kambini ambapo amekuwa akichukua matukio mbalimbali katika kambi yao kwa ajili ya kurusha kwenye kituo cha Televisheni cha Clouds.
Guetano Kagwa ambaye ni MCwa shindano hilo na Rena Calist Mkurugenzi wa Miss East Africa wakiwa katika picha ya pamoja na warembo hao mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo leo.
Kaka,
ReplyDeleteKwani hawakuwahi kuvaa mavazi ya UFUKWENI kaka?
Mbona unatuBANIA kaka bana?
Tadhali