Mwanamuziki
Koffi Olomide akijimwaya mwaya kwa madaha kabisa jukwaani usiku huu
kwenye tamasha la Tusker Carnival,huku akishangiliwa na umati mkubwa
watu uliohudhuria tamasha hilo.
Mwanamuziki
mahiri ndani ya kundi la Quartie Latin aitwae Cindy, linaloongozwa na
nyota wa muziki wa dansi kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akiimba
jukwaani usiku huu mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa wingi (hawapo
pichani),kwenye tamasha la usiku wa Tusker Carnival ndani ya viwanja
vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Pichani juu na chini ni Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide sambamba na skwadi lake la Quartie Latin
Koffi
Olomide akimtambulisha rafiki yake mkubwa jukwaani,Mkurugenzi wa Clouds
Media G Joseph Kusaga,ambaye ndiye aliyemleta hapa nchini kwa udhamini
mkubwa wa kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha
Tusker,ambapo pia mwanamuziki huyo alimshukuru sana Joseph kusaga kwa
ukarimu wake.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group,akizungumza machache na kuwashukuru sana
wadhamini wa onesho hilo sambamba na wadau mbalimbali waliojitokeza kwa
wingi kwenye onesho hilo ambalo limefana kwa kiasi kikubwa.
Koffi Olomide akimtambulisha mwanamuziki wake mahiri Cindy mbele ya mashabiki wake
Koffi Olomide akiimba jukwaani na madansa wake kwa umahiri mkubwa
sehemu ya umati wa washabiki wa onesho la Tusker Carnival wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri jukwani.
Koffi
Olomide akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya
Serengeti,Steve Gannon ambao ndio wadhamini wa onesho lake,anaeshuhudia
kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Medai Group,Joseph
Kusaga
Pichani juu na madensa wa Koffi Olomide wakiwajibika jukwaani vilivyo
Sehemu ya umati wa mashabiki wakifuatilia onesho
Palinogaje sasa na madensa wa Koffi Olomide
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya SBL,Steve Gannon akielekezwa jambo na
Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide kabla ya kupanda jukwaani.
Mwanamuziki
wa Kimataifa Koffi Olomide akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi
wa Kampuni ya SBL,ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho la mwanamuziki
huyo,aliyefanikiwa kuzikonga nyoyo za washabiki wake kwa kiasi kikubwa
usiku wa leo kwenye viwanja vya lidaz,Kinondoni jijini Dar.Koffi Olomide
siku ya jumapili atatumbuiza kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini
Mwanza.
Mwanamuziki Kalala JR akiliongoza jahazi lake la Twanga Pepeta jukwaani usiku huu.
Wanamuziki
wa Bendi ya Skylight wakionyesha umahiri wao wa kulishambulia jukwaa
kwenye Tamasha la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja
vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Wanamuziki
wa Bendi ya Diamond Musica wakifanya mambo yao jukwaani kwenye Tamasha
la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja vya Leaders
Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Madansa
wa Bendi ya Twanga Pepeta wakiwachengua Mashabiki wao wakati wa
muendelezo wa Tamasha la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye
viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru
(katikati),Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Nandi
Mwiyombela na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacoma Tanzania,Kelvin Twissa
wakibadilishana mawazo wakati wa muendelezo wa Tamasha la Tusker
Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja vya Leaders
Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Wadau.
Shangwe kwa Mashabiki wa Muziki wa Dansi jijini Dar.
Mdau akigonga vitu huku akiwa kaweka pochi yake mkononi.
No comments:
Post a Comment