Hoteli ya kitalii Ikondolelo
Lodge iliyoko Kibamba Jijini Dar es salaam , Imeteuliwa na Bodi ya mashindano
ya Miss Utalii Tanzania kuwa Hotel Rasmi ya mashindano hayo Mwaka huu 2012.
Mchakato wa uteuzi ulihusisha
Hotel zaidi ya saba zilizo jitokeza kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii
Tanzania 2012.
Kwa Ikondolelo kuwa hotel
Rasmi Miss utalii Tanzania itatumia zaidi ya Shilingi za kitanzania Milioni mia
moja , ikiwa ni udhamini wa gharama za kambi ya Warembo na waandaaji zaidi ya sitini(60)
kwa muda wa wiki tatu.
Bodi katika kuteua hotel rasmi
ya mashindano mwaka huu imezingatia Vigezo vifuatavyo:
Usalama wa watu na mali zao,
ubora wa viwango vya huduma ambayo siyo chini ya hadhi ya nyota (3) , mazingira
a hotel na utulivu wa eneo husika kulingana na viwango vya kitaifa na Kimataifa
vya mashindano ya Miss Utalii,pia kwa kuzingatia viwango vilivyo wekwa na
serikali kupitia Baraza la sanaa la Taifa (BASATA).
Warembo kutoka mikoa yote ya
Tanzania na Vyuo vikuu , wakiwa kambini katika Hotel ya Ikondolelo watafanya
shughuli mbalimbali za maandalizi na za kijamii; zikiwemo , Kujifunza kuogelea
katika bwawa lililopo hotelini hapo, Upigaji wa piga za minato katika bustani
zinazo zunguka hoteli, watapewa mafunzo maalum ya kutumia maeneo na vifaa
mbalimbali vya hotel za kitalii. Aidha washiriki wa fainali za taifa za Miss
utalii 2012 watapewa mafunzo kuhusiana na utalii, utamaduni, uwekezaji,
mazingira,afya ya jamii,elimu ya jamii uzalendo,watafundishwa mbinu za
kujieleza, kujiamini na kufanya matangazo.
Mkurugenzi mtendaji wa
Ikondolelo Lodge Ndugu Fredy Selekwa ameishukuru Bodi ya Miss utalii Tanzania
kwa kuwapa fulsa ya kuwa hotel Rasmi ya Mashindano haya muhimu kwa taifa katika
kukuza secta ya utalii na uchumi kwa ujumla. Ameihakikishia washiriki na
viongozi watakao kuwa kambini kuwapatia huduma zote muhimu kwa kiwango cha
kimataifa
Imetolewa na
Hamisi .A. Mkongowale
Mratibu wa Matukio
No comments:
Post a Comment