Watu mbalimbali wakiwa wamelizunguka jenereta usiku huu.
Mwanamuziki kutoka DRC-Congo,JB Mpiana akitumbuiza jukwaani mara baada ya kupanda mnamo majira ya saa tisa kasoro,baada ya hitilafu za umeme kwenye jenerata kurekebishwa.
SHOO
YA UZINDUZI WA ALBAM YA PILI YA MASHUJAA BAND, ILIINGIA DOSARI NA KUTAKA KUSHINDWA KUFANYIKA
KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB USIKU HUU KUTOKANA NA KATIZO LA UMEME LA
MARA KWA MARA LINALOSABABISHWA NA JENERETA LINALOTUMIWA KUTOA UMEME
KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,JIJINI DAR.
HALI HIYO IMEPELEKEA MMILIKI WA BENDI YA MASHUJAA,MAMA SAKINA KUPOTEZA FAHAMU NA KUKIMBIZWA HOSPITALI.
HADI SASA HAIJAFAHAMIKA KUWA HALI YAKE IKO VIPI KWANI HAKUNA TAARIFA ZOZOTE JUU YAKE.
MAFUNDI
BADO WANAENDELEA NA MAREKEBISHO YA JENERETA HILO NA IWAPO LITAKAA
SAWA,BASI NI MOJA KWA MOJA BENDI YA WENGE BCBG NDIO ITAPANDA
JUKWAANI,CHINI YA MKONGWE JB MPIANA.
TUTAENDELEA KUJUZANA KADRI MAMBO YATAKAVYOKUWA YAKIENDELEA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment