December 15, 2012

FM ACADEMIA YASHEHEREKIA MAIAKA YAKE 15 YA KUTOA BURUDANI

Rais wa bendi ya FM Academia Bw. Nyoshi El Saadat na waliokuwa wakurugenzi wa bendi hiyo miaka ya nyuma Abas Mwinyi Sadamu Hussein kushoto na Felician Chaula kulia kwa Nyoshi El Saadat pamoja na warembo mashabiki wa bendi ya FM Academia wakikata keki kwa pamoja, wakati sherehe ya Bendi hiyo kutimiza miaka 15 ya huduma yake katika kutoa Burudani nchini Tanzania, iliyofanyika kwenye klabu ya Msasani jijini na kuambatana na onyesho kubwa na la kukata na shoka lililoshirikisha Mashabiki, Wadau na watu wa karibu na bendi hiyo , huku Fullshangweblog ikikumuvuzishia moja kwa moja matukioa ya onesho hilo.

Onesho la bendi ya FM Academia kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake gaoa nchini linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
Wakurugenzi wa bendi hiyo miaka ya nyuma Abas Mwinyi Sadamu Hussein kushoto na Felician Chaula suti nyeusi wakifungua shampeni wakati wa hafla hiyo. Hii ndiyo keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya hafla hiyo
Mwanamuziki Jose Mara wa bendi ya Mapacha Watatu ambaye pia aliwahi kuwa mwanamuziki wa bendi ya FM Academia akifanya vitu vyake na bendi yake.
Vimwana wa bendi ya Mapacha Watatu wakifanya vitu vyao jukwaani.
 
Hapa mzuka wa muziki umepanda na uko juu sana kama unavyoona.
 
Baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo hawakuwa nyuma kulisakata Sebene la FM Academia kama wanavyoonekana.
Vijana wa FM Academia wakifanya vitu vyao jukwaani usiku huu kwenye ukumbi wa Msasani Club jijini Dar es salaam,
Vijana wa FM Academia wakifanya vitu vyao jukwaani usiku huu kwenye ukumbi wa Msasani Club jijini Dar es Salaam. PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM

No comments:

Post a Comment