Nafasi Ya Matangazo

December 25, 2012

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akiangalia nguo zinazoshonwa na kikundi cha ushonaji kilichopo kijiji cha Bugalama wilayani Geita ambacho kimenufaika na mkopo wa shilingi milioni mbili kutoka mfuko wa maendeleo wa halmashauri hiyo. Waziri Dk. Mukangara alitembelea kijiji hicho jana ili kuona fedha za mkopo zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Nyakalalo kililopo kijiji cha Kitigiri wilayani Geita, Gideon Msabila (kushoto) ambaye alimuelezea jinsi walivyonufaidika na mkopo wa mfuko wa maendeleo ya vijana fedha ambazo zimewawezesha kufungua duka la rejareja la bidhaa za nyumbani.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Geita, Kata ya Bukondo na kijiji cha Kitigiri mara baada ya kumaliza ziara yake katika kijiji hicho jana ili kuona fedha za mkopo za mfuko wa maendeleo ya vijana zimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
Vijana wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka katika kijiji cha Kitigiri wakifurahia fedha shilingi 50,000/= walizopewa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia) kwa ajili ya kununulia soda za sikukuu ya Krismasi . Waziri Dk. Mukangara aliwahimiza vijana hao kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza kuzalisha chakula kwa wingi zaidi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia) akiongea na vijana wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka kilichopo kijiji cha Kitigiri wilayani Geita umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza kuzalisha chakula kwa wingi zaidi .
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Bodaboda kilichopo kijiji cha Bugalama wilayani Geita, Enos Komanya wakati alipotembelea kikundi hicho ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo wa halmashauri. Waziri Dk. Mukangara alitembelea kijiji hicho jana ili kuona fedha za mkopo zilizotolewa na mfuko wa maendeleo ya vijana zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha.
Posted by MROKI On Tuesday, December 25, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo