MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia Ikwene (24)
Warembo mbalimbali wanaoishi Ulaya na walioshinda katika mashindano ya Miss East Africa huko Ulaya pia watashiriki katika mashindano ya Miss East Africa 2012 yatakayofanyika tarehe 07 December katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam warembo hao ni:
1. MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia Ikwene (24)
2.MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg Marcos (21)
3.MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona Ruboneka (24)
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.
MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona Ruboneka (24)
MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg Marcos (21)
No comments:
Post a Comment