HABARI kutoka Chuo Kikuu cha Kampala Tawi la Dar es Salaam Tanzania,
zinapasha kuwa Wahadhiri na wafanyakazi wa Kawaida wa chuo hicho wameingia katika
mgomo kuanzia leo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi chuoni hapo
na kuifikia meza ya Father Kidevu Blog, wanadai kuwa Wahadhiri hao wameanza mgomo wao leo wa kutoingia madarasani
kufundisha kufuatia madai yao ya mishahara na posho nyingine.
Wanafunzi hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao wanasema kuwa walihao
walikaa kikao jana na kufikia muaafaka huo wa kuingia katika mgomo wa kudai
mishara yao na hawatoingia madarasani hadi pale watakapolipwa fedha zao hizo.
“Awali tulikuwa tukisikia kuwa wanadai mishara ya miezi mitano yaani
tangu mwezi mei hawajalipwa lakini kwa mujibu wa taarifa zilizo samba chuoni hapo
leo ni kuwa madai ya wahadhiri hao yalioyobaki hadi sasa ni ya miezi miwili.” Alisema
Mwanafunzi huyo.
Wanafunzi hao walidai kuwa kuwepo kwa mgomo huo kutawaathiri kimasomo
kwani wapo baadhi yao wanaoingia katika kufanya mitihani hivi karibuni na
wanafunzi wa mwaka wa kwanza ndio kwanza wameripoti chuoni hapo hivyo
wanahitaji kupata mafunzo zaidi na si kukutana na migomo hiyo.
No comments:
Post a Comment