Taarifa
zilizopatikana jioni ya leo zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa muigizaji
katika kikundi cha Kaole,(pichani enzi za uhai wake) ,aliyekuwa
akitambulika kwa jina la Mlopelo amefarika dunia mapema leo hospitali ya
Temeke,jijini Dar,kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu wameitonya
Blog ya Jiachie kuwa Marehemu Mlopelo amefarika mchana wa leo kwenye
hospitali ya Temeke mapema mchana wa leo, na kwamba shughuli zote za
Msiba zipo nyumbani kwao Temeke Wailess mtaa wa Boko,imeelezwa kuwa
mazishi yake yatafanyika mapema kesho saa nne.Wadau
Taarifa kamili tuvute subira kidoogo tutakuja juzana hapa hapa jamvini
tena.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amen.
No comments:
Post a Comment