Amakweli ukisikia
kukua kwa demokrasia nchini ni huku… wale vijana wawili maarufu na makada wa
Chama cha Mapinduzi kutoka Wilkayani Nzega, Hussein Bashe na Dk Hamis
Kigwangala ambao wakati wa chaguzi za ndani za Chama hicho walikuwa ni mahasimu
wakubwa hivi sasa mambo yao ni super na wanapiga stori kama kawaida.
Kamaera ya Father
Kidevu Blog iliyopo ndani ya Ukumbi na viwanja vya Ukumbi wa Kizota mjini
Dodoma unakofanyika mkutano Mkuu wa 8 wa chama hicho umewanasa makada hao
wakipiga stori na kucheka kwa kwenda mbele.
Wakiwa hawana
habari juu ya kuchukuliwa taswira zao na baada ya kugundua hilo walimueleza
Mpiga picha Mroki Mroki kuwa wao wako poa kabisa na maneno ya watu tu kiuwa
mimi (Bashe) siongei na Dk. Kingwangala.
Bashe (kushoto) akizungumza jambo huku wakiwa katika furaha na Kanda mwenzake wa CCM Nzega na Mbunge wa Nzega, Dk Kingwangala nje ya ukumbi wa Kizota wakati Makundi mbalimbali ya Mikoa yakipiga picha na Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment