November 13, 2012

MABADILIKO MAKUBWA YA SECRETARIETI YA CCM YANUKIA LEO

Mkutano Mkuu wa nane wa Chama Cha Mapindsuzi (CCM) ulioanza juzi, Novemba 11, unafikia kilele chake leo Novemba 13, 2012.

Kulingana na ratiba zilizopo, katika kikao chake chini ya Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete, yatafanyika mambo kadhaa kuuhitimisha mkutano huo, ikiwa ni pamoja na kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC viti kumi Bara na kumi Zanzibar uliofanyika juzi.

Mtokeo hayo ya NEC yatatangazwa rasmi huku kukiwa tayari kuna tetesi za kutajwa majina ya washindi hasa kwa upande wa Bara amabapo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Uratibu na Mahusiano, Steven Wasira ametajwa kuongoza kwa kura akifuatiwa na Januari Makamba, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigella.

Mbali na kutangazwa matokeo hayo, utafanyika uchaguzi wa Makamu Mweneyekiti wa CCM (Bara) na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ambao tayari wanaowania nafasi hizo wameshatangazwa kwenye mkutano huo kuwa ni kwa upande wa Bara ni Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Phili Mangula na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa upande wa Zanzibar.

Pia wajumbe watafanya uchaguzi kumpata Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, ambapo anayegombea nafasi hiyo, ni Mwenyekiti wa sasa, Rais Kikwete na inatarajiwa kwamba atapata kura za kishindo kutokana na kuonyesha kusimamia vema utekelezaji wa ilani ya CCm katika nyanja mbalimbali wakati ya uongozi wake.

Bila shaka safu ya uongozi wa CCM ngazi hiyo ya Kitaifa, itakamilishwa kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuteua Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti mpya, ambapo dodoso zinaonyesha kwamba huenda yakafanyika mabadiliko kutoka sekretarieti ya sasa.

Katika Sekretarieti ya sasa inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama, waliomo ni Makatibu wa NEC:- Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Jauaniari Makamba na Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba.

Pia mabadiliko hayo huenda yakapanga upya safu ya Manaibu Katibu Mkuu wa CCM wa Bara na Zanzibar ambao kwa sasa Bara ni John Chiligati na Zanzibar ni Vuai Ali Vuai.

Kwa mujibu wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye jumla ya wajumbe 2,218, wamehudhuria mkutano huo Mkuu wa nane wa CCM ambao wengi wameuelezea kuwa mwaka huu umekuwa wa kipekee na wa kihistoria kutokana na maandalizi yake yaliyofanywa chini ya Idara ya Nape.

No comments:

Post a Comment