Nafasi Ya Matangazo

November 28, 2012

SIKUDHANI hata kidogo kama Jumatatu ya Novemba 26, 2012 majira ya saa moja niliposimama kwa muda mrefu katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere zamani Pugu na kuangalia matangazo kadhaa ya bidhaa za Azam na kuchezwa kwa ufasini mkubwa na Sharo Milionea na Kig Majuto ndo nilikuwa naangalia maisha ya msanii huyo akiwa ana pumzi.

Baadhi ya matangazo yalinivutia na kunifanya nicheke hasa lile la Boti ambalo Majuto na Mkewe walienda kumpokea kijana wao akitoka Zanzibar na alipo tua akaanza midondo yake huku akijifuta bega na kumfanya Majuto aliyevalia suti nae kumfatisha.

Dah! Nikiwa mbele ya Komputa yangu nikiendelea na kazi za Kublogua majira ya saa tatu kasorobo hivi nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu Abdalah Msuya akitaka kufahamu ukweli juu ya ajali na kifo cha Sharo Milionea.

Mh! Nilistuka nikamwambia sijasikia lolote na ndio kwanza nimewasha mashine nataka kufanya updates za Blog yangu ya www.mrokim.blogspot au FATHER KIDEVU BLOG, lakini nikamwambia nipe dakika chache, nikawasiliana na blogger mwenzangu Ahmad Michuzi nae akaniambia amezisikia ila bado si za uhakika.
 
Pole nazituma Faza, mlo wafuasi wa Sharo,
Pole zifike Muheza, mlio mlea wetu Sharo,
Hili siwezi libeza, mlaaniwe mlomwibia Sharo,
Pole kwa tasnia ya filamu, kwa msiba huu wa Sharo.

Uchekapo huongeza siku, Sharo tunakushuru sote,
Binafsi uliongeza buku, ukanifanya sebleni nisitoke,
Mama alileta na kuku, ukatufanya kutwa tucheke,
Pole kwa tasnia ya mziki, kwa msiba huu wa Sharo.


Niliamua kumpigia simu Kamnada wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Costantine Massawe na kuniambia ni kweli kuna ajali imetokea Muheza kijiji cha Lusanga na kumhusisha msanii Sharo Milionea ila bado hajapata ripoti kamili na baada ya dakika chache niwasiliane nae.
 
Nilivuta subira ya dakika tano hadi kumi kasha nika mpigia tena simu Kamishna Msaidizi huyu wa Polisi na kunipa jibu kuwa Nikweli Sharo Milionea amefariki katika ajali ya gari majira ya saa mbili usiku.

Hakika ni majonzi kwa kila mtanzania mpenda sanaa ya maigizo, vichekesho na filamu achilia mbali mziki hapa nchini na ukanda wote wa afrika mashariki kufuatia kifo cha Hussein ramadhani Mkieti ama Sharo Milionea.

Ni majonzi makubwa sana maana hasa ukiangalia kifo chake kilivyo tokea kwa msanii huyu, ambaye alikuwa safariki akitokea jijini Dar es Salaam kwenda nyumbani kwao Lusanga Muheza Tanga kuwasalimu wazazi na akiwa ndio amekanyaga ardhi ya eneo alilozaliwa la Lusanga akakutwa na umauti kufuatia ajali ya gari.

Mziwanda huyu katika familia ya watoto watatu wa Mzee Ramadhani na Zainabu Mkieti, aliyezaliwa mwaka 1987 katika kijiji cha Lusanga, Muheza, Tanga.

Sharo Milionea alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Lusanga na baadaye kujiunga na sekondari ya Kwabutu alikosoma hadi kidato ya tatu alopoacha shule kutokana na matatizo ya kifamiliaa mabyo huwakumbuka vijana na watoto wengi duniani kote.

Sharo baada ya kuacha shule mnamo mwaka 2003 aliamua kuhamishia maisha yake jijini Dar es Salaam ambako mama yake mzazi alikuwa akiishi na hii ni baada ya kuona mambo kule Lusanga hayasomeki na kuamua kwenda mjini kupambana.

Akiwa jijini Dar es Salaam, Sharo alijifunza vitu mbalimbali ambavyo wenyeji wake walidhani vingemkwamua kimaisha hasa kutokana na elimu ndogo aliyonayo, miongoni mwa vitu hivyo ni kujifunza umakenika na utengenezaji wa majokofu na ikawa haitoshi na kufanya biashara ya magazeti maeneo ya Kiwalani.

Mama yake aliamua kurejea Muheza kwenda kumuuguza bibi yake na kujikuta akiishi peke yake katika jiji hili la Dar es Salaam.

Lakini kuingia kwake katika sanaa ni katika kuhangaikia tumbo, na mtu aliyemsukuma sana marehemu Sharo Milionea kuingia katika sanaa ni Siasa Mohamed a.k.a Chiba.

Kundi la kwanza kuundwa na lilikuwa ni kati ya Sharo, Snura Mushi, Nas na Dats na hii ilikuwa mwaka 2005 walipo unda kundi hilo la mziki ambalo hata hivyo halikudumu baada ya mmopja wao Snura kuhamia maigizo na kucheza filamu ya Jumba la Dhahabu.

Baada ya kuona mwenzao amecheza filamu hiyo Sharo nae alikacha kundi hilo na kuahamia katika kundi la Sanaa za maigizo la Jamal Arts lilikuwa chini ya Gumbo Kihorota na kuonesha makali yake katika filamu ya Zinduna na Itunyama ambayo aliigiza pamoja na wakali wengine wa vichekesho wanaotamba na kundi la Ze Komedi Origino, Emmanule Mgaya ‘Masanja, Alex Charamila ‘Macklegan’,.

Historia ya Marehemu Sharo Milionea ilizidi kupanda na kuanza kujipatia umaarufu na kwa mara ya kwanza alichukuliwa na Musa Kilali na aliigiza kwenye filamu ya vishekesho ya Mbwembe vol 2 ambayo aliigiza kama ’Bitoz ’ wa kijijini huko nako aliigiza na wasanii kadhaa wakiwamo Robert Augustino ‘Kiwewe’ na Christian Masele ‘Masele’.

Baada ya kufanya vizuri licha ya uchanga wake Msanii mwenzake wa Vichekesho, Kiwewe alifanya utaratibu na kumuingiza katika filamu ya vichekesho iliyokwenda kwa jina la ‘Vichwa Vitatu’.

Alifanikiwa kuigiza filamu hiyo na baade kuigiza filamu zake za Vichekesho za za Sharobalo na Sharo Milionea.

Miaka ya hivi karibuni Marehemu aaliingia mkataba mpya kwa kipindi cha mwa mwaka mmoja na Khalfan Abadallah anayemiliki Kundi la Bongo Super Stars Comedy ambalo linawashirikisha waigizaji kadhaa akiwamo Kign Majuto na Masele, pia aliigiza komedi ya Back from New York na Mtoto wa Mama.

Ni hapo ndipo maneno ya Oh! Mamaa na Kamata Mwizi Meen yalipoanza kuvuma wakati wa filamu ya mtoto wa mama ikiwa sokoni.

Sharo Milionea hakika alikua hana tofauti na Mcheza Filamu maarufu diani Will Smith ambaye anaweza kuigiza komedi, filamu  na kuimba.

Binafsi naweza kusema kuwa miongoni mwa wasanii walio weza kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu na Ucheshi ni Sharo Milionea maana awali ilizoeleka kuwa ili mtu achekeshe lazima avae nguo za ajabu lakini kumbe hata ukivaa smati inawezekana.

Umautio unamfika kijana huyu wakati tayari akiwa amesha shika chini vizuri na sanaa yake ina mea vilivyo katika anga mbalimbali na kujipatia tenda na kazi nyingi za matangazo akiwa na nguli King Majuto.
 
Sharo Milionea ambaye alionekana na kuzoeleka kuwenye komedi, lakini pia aliweza kuubebea uhusika wake vizuri katika filamu inayotamba sana ya Chumo iliyoongozwa na Jordan Riber yenye maudhui ya kupambana na ugonjwa wa malaria.

Akiwa ameigiza kwa jina la Juma katika filamu hiyo, Sharo Milionea alicheza kama kijana masikini na ametokea kumpenda Amina (Jokate Mwegello), ingawa baba yake Amina Ali alitaka binti yake kuwa na maisha mazuri, hivyo kutaka aolewe na Yustus (Yusuph Mlela) ambaye aliyetoka kwenye familia ya kitajiri.

Mbali na kucheza filamu Marehemu Sharo Milionea alikuwa na ushirikiano mzuri na wasanii wengine na hata kushirikiana nao kama alivyo fabya katika wimbo wa ‘Sababu ya Ulofa” wa msanii Top C.

Kama ilivyo ada jina la utani mtu hajipi mwenyewe bali hupewa na watu kama si marafiki bali ni mashabiki wa kazo zako, hata mimi Father Kidevu si kujipa bali nilipachikwa tu na wa fanyakazi wenzangu pale The Guardian Limited kwa staili yangu ya ndevu.

Hivyo chanzo cha jina la Sharobalo, ni mashabiki wake kutokana na staili yake ka kibrazamen na wale walio kuwa nae watakumbuka kuwa Sharo Milienea tangu akiwa ndogo huko Tanga suala la usafi lilikuwa jadi yake na hata kama alikuwa na nguo mbili basi zitazifua, ilimradi aonekane nadhifu.

Aliamua kubadili jina hilo la utani kutoka Sharobalo hadi Sharo Milionea baada ya msanii mwenzake Bob Junior kudai ni mali yake na linatumika katika studio yake Sharobalo Recods hivyo akaamua kujiita Sharo Milionea.

Katika uhai wake Sharo Milionea muasisi wa Ooh! Mama na kamata Mwizi meen huku ukijifuta bega na kuvuta mguu mmoja ukiwa umekamatia suruali yako katika flaizi aliwahi watamka kuwa anawazimikia sana Joti na King Majuto ambaye sasa hadi umauti unamkuta walikuwa wakifanya kazi pamoja.
 
Akiwa na King Majuto pia Sharo Milionea alicheza Filamu ya ‘Alosto’ akiwa na mkongwe huyo na majuto kuonesha kipaji chake licha ya umri alionao.

Nilisikiliza mahojiano ya Clouds FM na King Majuto kufuatia kifo cha Sharo Milionea, japo ni huzini lakini nitaka kucheka pale Majuto aliposema baada ya kupata taarifa za msiba mwili wake ulifutuka kama pulizo na mishipa ilijaa.
Dah! Kweli inauma sana dhahiri tulimpenda sana Sharo miliomnea lakini ndop hivyo mauti yamemfika na kutuacha mashabiki wake wanyonge, kama ilivyo ada tutaendelea kuwa na imani kuwa tutaonana nao tena wapendwa wetu hawa.

Sharo Milionea alikuwa na kiu ya siku moja kuigiza na wakali wa vichekesho na vituko kama Mr Bean, Eddy Murphy na Will thimis, na ni wasanii wa majuu alikuwa anazimia sana kazi zao na alikuwa haishi kuziangalia.

Sharo alikuwa na ndoto pia ya kuwa Muigizaji wa kimataifa na mfanya biashara, lakini zote hizi ndoto zake zimeyeyuka kutoka na kifo kuchukua uhai wake. 

Leo hii Father Kidevu Blog hatuna jipya la kusema dhidi yako Sharo Milionea zaidi ya kusema kapumzike kwa amani, na hakika kama kucheka na kufurahi kunaongeza siku za kuishi duniani basi uliongeza sana salio letu la kuishi huku salio lako likikosa muongezaji. 

Posted by MROKI On Wednesday, November 28, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo