November 15, 2012

MTOTO SELEMANI SAID ANAHITAJI MSAADA WAKO

MILIONI sita zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Selemani Said (1), ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku ukiwa nje ya tumbo lake imeleezwa.
Akizungumza na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent ambaye ni Mkazi wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na sehemu ya kutolea haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa ikitokea mdomoni.

Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia katika kumfanyia operesheni mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso makubwa. Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.

“Mimi ni nachoomba ni msaada wa fedha ili niweze kumpeleka kwenye matibabu kwani sina msaada wowote,ukichukulia wazazi wangu kufariki na hivi sasa naishi kwenye nyumba ya mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju wilayani Kinondoni jijini baada ya kushindwa kupangisha chumba kwani sina kazi yeyote”alisema.

Aidha, alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje, ni baada ya kufanyiwa operesheni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo hata alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa madaktari na wahudumu wengine.

Alisema kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia anaweza wasiliana naye kwa kupiga simu namba o715 83 77 00, na namba ya mwenyekiti huyo wa mtaa 0656780236.

Veronika ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Kijiji cha Uru,Moshi ambaye alimzaa mtoto huyo na mwanamme aliyemtaja kwa jina la Abdalah Said, kabilake makonde mfanyabiashara wa viatu Ubungo.

No comments:

Post a Comment