Pichani
ni muonekano wa namna tairi la kushoto la basi la Arusha Express (lenye
usajili wa namba hizo hapo chini) lifanyalo safari zake kutoka Dodoma
kwenda mkoani Kilimanjaro (Moshi) kupitia Babati limepata ajali maeneo
Makuyuni likielekea mkoani Kiliamanjaro mapema jioni ya leo,ambapo tairi
lake lilipasuka na kuacha njia,katika ajali hiyo hakuna aliyefariki
zaidi ya Majeruhi kadhaa ambao walipelekwa hospitali ya Mount Meru kwa
matibabu.
Basi
la Arusha Express kama lionekanavyo mara baada ya kupata ajali,Basi hilo
lilifanikiwa kuanguka hapo baada ya kukumbana na mti mkubwa kama
uonekavyo chini ya basi hilo.
Baadhi
ya abiria waliokuwa kwenye basi la basi la Arusha Express akielekea
kwenye basi lingine la kampuni hiyo hiyo.liendalo Arusha ambamo Mzee wa
Jiachie alikuwepo na kufanikiwa kuzinasa picha hizi mda mfupi mara baada
ya ajali kutokea.Aidha abiria hao walisema kuwa pamoja na tairi la basi
hilo kupasuka,chanzo kikubwa ilikuwa ni mwendo kasi wa Dereva ambaye
walimkanya kupunguza mwendo,lakini yeye alikuwa akikaidi maneno ya
abiria wake.
Basi la Arusha Express kama lionekanavyo kwenye korongo baada ya kuanguka. SOURCE: JIACHIE BLOG
No comments:
Post a Comment