November 13, 2012

MATOKEO YA WAJUMBE WA NEC YATANGAZWA

MATOKEO  ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC katika kura zilizopigwa juzi mjini Dodoma katika mkutano wa  nane wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yametangazwa.

Akitangaza matokeo hayo Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mjumbe wa NEC, Spika wa Bunge Anne Makinda amewataja walioshinda nafasi hizo ni kama ifuatavyo. 

Walioshinda nafasi 10 Zanzibar:
Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Wengine  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto.

Walioshinda nafasi 10 Bara
Majina ya wajumbe wa Nec walioshinda bara na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (2012), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824).

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana  na Michezo, Fenela Mukangara (984).

Awali matokeo haya yalivuja siku moja kabla isipokuwa kukosewa kwa kura za Mchemba pekee.
 Wajumbe wa Mkoa wa Mtwara
 Wajumbe wa Singida mambo ni safi
 Wajumbe wa Tanga
 
 Morogoro wapo
 Huko Kagera nao wapo
 Mwanza nao wapo
 Wajumbe wa mkutano
 Viongozi wa Serikali
 Kutoka Singida
 Wajumbe kutoka Iringa

Wajumbe kutoka mkoa wa Geita wakiwa mkutanoni.

No comments:

Post a Comment